logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa afariki kwa kitanda cha 'sidechick' baada ya kuondoka kwa mkewe 5am kwenda ku'cheat

“Rafiki wa familia ndiye aliyempigia simu mke na kumpa taarifa hizo."

image
na Radio Jambo

Makala16 May 2023 - 07:21

Muhtasari


• Rafiki wa familia ndiye aliyempigia simu mke na kumpa taarifa hizo.

• Mke hakuamini mpaka alipoona mwili usio na uhai. Siku ya huzuni iliyoje.

Mwili wa marehemu

Mwanaume mmoja ambaye aliamua kwenda kujiburudisha na mpango wake wa kando aliripotiwa kufariki muda mfupi baada ya kufika katika nyumba hiyo.

Kulingana na taarifa ambazo zilichapishwa Twitter na wakili mmoja, mrembo huyo anafanya kazi katika shirika la huduma ya vijana kwa taifa NYS.

Kwa mujibu wa wakili huyo kwa jina @bolanlecole kwenye Twitter, marehemu aliondoka nyumbani mwendo wa saa kumi na moja alfajiri kwenda kumtembelea mrembo huyo kwa ajili ya kufanya mapenzi ya haraka lakini cha kusikitisha aliaga dunia wakiwa bado wanaendelea na tendo.

Alisema mke wa marehemu alishindwa kuamini kuwa mumewe amefariki hadi alipoiona maiti yake.

Alitweet;

"Mwanamume alimwacha mkewe kwenye kitanda chao cha ndoa mwendo wa saa 5:30 asubuhi na kufululiza hadi kwa nyumba ya kijana wa NYS ambaye alikuwa na uhusiano naye na kufariki akiwa katika shughuli za utumishi wakati akitekeleza wajibu wa ziada wa ndoa.”

“Rafiki wa familia ndiye aliyempigia simu mke na kumpa taarifa hizo. Mke hakuamini mpaka alipoona mwili usio na uhai. Siku ya huzuni iliyoje.”

Taarifa hiyo iliwaacha watumizi wa Twitter na maswali mengi baadhi wakijaribu kuweka kwenye mizani kuhusu ni nini wangefanya wangejipata katika hali kama hiyo ya mkewe.

“Mungu amekataza hilo. Lakini kama ningekuwa mke wake, sitaburuta kesi yoyote, kwa sababu inamtumikia sawa. Nitaweka tu mikono kwenye kidevu kwa kuangalia,” mmoja alisema.

“Hisia mchanganyiko kwa mwanamke, atakuwa na hasira kwa sababu alikufa juu ya mwanamke pia kuwa na huzuni kwa sababu alipoteza mume wake💔💔💔” mwingine kwa jina Naom alisema.

“Mimi ningekuwa mkewe ningeambia yule mwenye alinipigia simu kunitaarifu afikishe habari hizo kwa wazazi wake ili waende kutambua mwili wa mtoto wao,” Mwingine alisema.

Ungekuwa mke wa marehemu, ungefanyaje?

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved