Hasira Hasara! Vitendo vya wanawake wanapowakamata wapenzi wa wakiwasaliti kimapenzi

Hasira ya wanawake baada ya kuwapata wapenzi wao wakiwasaliti kimapenzi huwafanya kuchukua hatua za kutisha.

Muhtasari

• Mwanamke anapompata mwanamume wake akimsaliti kimapenzi basi bila shaka kuna vitendo vya ghadhabu ambavyo hufanya.

Mwanamke anapompata mume wake akimsaliti kimapenzi basi bila shaka kuna vitendo vya ghadhabu ambavyo hufanya haswa ikiwa amempata hadharani.

Baada ya Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi kupost katika akaunti yake ya Twitter kuhusu mwanamke aliyempata mchumba wake akimsaliti kimapenzi na matukio yaliyofuata hadi kesi kufikia mahakamani, tumekuandalia orodha ya baadhi ya vitendo vya ghadhabu ambavyo wanawake hufanya wakiwapata wachumba wao wakiwasaliti kimapenzi.

1. Kuvunja televisheni au redio iwapo mwanamume huyo ako nazo.

2. Kuharibu gari la mpenzi wake.

3. Kuchoma nguo za mpenzi wake.

4. Kuvunja simu.

5. Kumwaga maji kwa godoro yake.

6. Kuvunja vyombo vya nyumba kwa mfano, meza, vikombe, sahani na kadhalika.

7. Kujaribu kupigana na mwanamume huyo na kusababisha drama

8. Iwapo anajuana na wazazi wa huyo mpenzi wake haswa mamake, basi atawapigia simu na kuwaelezea chenye amefanywa na kijana wake

9. Kujaribu kujiua.

Kama una zingine, jisikie huru kuongeza. Orodha hii ilitengenezwa kwa haraka hivyo hatujaweka zote.