Mike Sonko kumsadia mwanamke aliyekamatwa na polisi baada ya kuharibu mali ya mchumba wake

Mwanamke huyo alikamatwa baada ya kuharibu mmali ya mpenzi wake baada ya kumkamata na mwanamke mwingine.

Muhtasari

• Mwanamke huyo anadaiwa kuharibu gari la mpenzi wake na kuvunja runinga yake alipompata mpenzi wake akiwa kwenye tendo hilo.

• Mike Sonko alichapisha kwenye akaunti yake ya Twitter kuashiria kutorithika na umauzi huo wa mahakama kuhusu suala hilo.

Sonko aonesha kiburi cha pesa Twitter
Sonko aonesha kiburi cha pesa Twitter
Image: Twitter

Mike Sonko amejitolea kusaidia mwanamke anayeshukiwa kuharibu mali ya mchumba wake.  

Mwanamke huyo kwa jina Imelda Mwendwa Kiguda alikamatwa Jumatatu kwa madai ya kuharibu mali ya mpenzi wake baada ya kumfumania na mwanamke mwingine.

Mwanamke huyo anadaiwa kuharibu gari la mpenzi wake na kuvunja runinga yake alipompata mpenzi wake akiwa kwenye tendo hilo.

Alipofikishwa kortini binti huyo alitakiwa kulipa dhamana ya pesa taslimu sh100,000.

Mike Sonko alichapisha kwenye akaunti yake ya Twitter kuashiria kutorithika na umauzi huo wa mahakama kuhusu suala hilo.

Katika ujumbe wake Twitter, Sonko alijitolea kulipa dhamana ya pesa taslimu na kuwaomba marafiki na familia ya mwanamke huyo kumtuma  nambari ya kesi hiyo mara moja.

"Hili halikubaliki kabisa, hebu marafiki na jamaa wa bibi huyu nitumie namba ya kesi mahakamani mara moja ili nimdhamini." sonko aliandika.

Sonko pia alisema kuwa atamlipa wakili yeyeto atakaye jitokeza na kumwakilisha mwanamke huyo kotini.

"Alafu, wakili yeyeto mwanamke achukue kesi hio na kumtetea huyu binti nitalipa malipo ya kisheria kwa niaba yake." Sonko aliongeza.