Ogopa Kanairo!Amira awashauri mashabiki husu kuwachumbia wanaume na wanawake wa Nairobi

Amira anapofikiria kuchumbiana tena au la, tayari amewafahamisha mashabiki wake kile anachotaka hasa kwa mpenzi wake ajaye.

Muhtasari
  • Moja ya mambo haya ni kuwa mwangalifu kuhusu uchumba Nairobi, kwa sababu inaonekana uwezekano wa mtu kuishia kuumia moyo  ni mkubwa sana.
Image: INSTAGRAM// AMIRA

Sio siri kuwa mfanyabiashara maarufu na mtengenezaji wa kidijitali Amira amekuwa peke yake kwa muda sasa.

Mama huyo  wa watoto wawili alitalikiana na mumewe wa zaidi ya miaka 15, mfanyabiashara  Jamal Marlow almaarufu Rohosafi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Sababu ya kuachana na ndoa hiyo ni kwa sababu alikuwa akimcheza mara kadhaa na hili ni jambo ambalo mara nyingi lilimfanya ahuzunike moyoni kwa muda mrefu zaidi.

Kama mtu mwingine yeyote huko nje ambaye ametoka kwenye ndoa iliyofeli, haswa yenye sumu, amejifunza jambo moja au mawili kuhusu baadhi ya mambo ambayo hatavumilia katika uhusiano wake ujao.

Moja ya mambo haya ni kuwa mwangalifu kuhusu uchumba Nairobi, kwa sababu inaonekana uwezekano wa mtu kuishia kuumia moyo  ni mkubwa sana.

Katika chapisho la hivi punde kwenye hadithi zake za Instagram, Amira alichapisha video fupi yake akiwa ndani ya gari akiimba wimbo, na akaisindikiza na nukuu inayoonya mtu yeyote kuwa mwangalifu ikiwa anataka kuchumbiana jijini.

"Sababu ya huzuni yako ni kwa sababu unajaribu kutafuta mapenzi katika jiji la Nairobi, jiji linalojulikana kwa trafiki na unywaji pombe," aliandika.

Amira anapofikiria kuchumbiana tena au la, tayari amewafahamisha mashabiki wake kile anachotaka hasa kwa mpenzi wake ajaye.

Mama wa watoto wawili anataka mwanaume ambaye atamlinda kama malkia alivyo.

Siku ya Alhamisi, wiki jana akiwa Dubai kwa ajili ya kufanya manunuzi, alichapisha video ya mwanamume ambaye alidai alikuja kumchukua kwenye gari aina ya Range Rover. Hata hivyo hakutoa maelezo wala sura ya mwanamume huyo.

"Anapokuja kukuchukua kwenye gari la Range Rover Vogue 2023 autobiography," Amira alisema kwenye video aliyochapisha.

Aliongeza, "Niskie mtu akisema amevaa socks na open shoes."

Mama wa watoto wawili wavulana alionyesha tu miguu ya mwanaume huyo asiyejulikana na ambaye anaonekana kuwa tajiri.