Wafahamu wanawake wenye watoto na msanii Diamond Platinumz

Baadhi ya wanawake hawa wenye watoto wa Diamond ni watu maarufu katika ukanda wa Afrika Masharariki.

Muhtasari

• Mwanamke mwingine ambaye ana mtoto na Diamond ni Mwanamziki Mkenya Tanasha Donna.

• Mmoja wa wanawake hawa maarufu ni mwanamitindo Hamisa Mobeto ambaye ni mama wa mtoto wa kiume.

Baadhi ya wanawake wenye wako na watoto na Diamond
Baadhi ya wanawake wenye wako na watoto na Diamond

Mwanamuziki Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platinumz kwa muda sasa ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuwa na watoto 6 ambao wametoka kwa mama tofauti.

Baadhi ya wanawake hawa wenye watoto wa Diamond ni watu maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mmoja wa wanawake hawa maarufu ni mwanamitindo Hamisa Mobeto ambaye ni mama wa mtoto wa kiume.

Mtoto huyo anafahamika kwa jina Dylan Naseeb.

Hamisa alizaliwa Mwanza, Tanzania tarehe 10 Desemba 1994.

Mwaka wa 2011, alishiriki katika shindano la urembo la Miss Indian Ocean 2011 ambako aliibuka nambari ya pili.

Mwaka wa 2012, alishiriki katika Miss University Africa na kufanikiwa kuwa miongoni mwa wanawake 10 bora.

2018, alishinda Mwanamitindo wa Kike wa Mwaka katika Tuzo za Swahili fashion Week. Mwaka huo huo Mobeto aliteuliwa kuwa mwenyeji wa shindano la Urembo la Miss Tanzania.

 Mwaka huo huo, aliteuliwa kuwa Mjasiriamali Bora wa kike Afrika Mashariki katika Tuzo za BEFFTA.

Desemba 2020, alishinda Mwanamitindo Bora wa Kike wa Kidijitali wa Mwaka 2020 katika Tuzo za Kidijitali Tanzania.

Mwanamke mwingine ambaye ana mtoto na Diamond ni Mwanamuziki Mkenya Tanasha Donna.

Tanasha Donna alizaliwa Kenya tarehe 7 Julai 1995 na mama Mkenya na Baba wa Kiitaliano.

Uhusiano wa Diamond na Tanasha ulizaa kazi ya muziki ya Donna baada ya kushirikiana katika wimbo wa 'Gere'.

Mama huyo wa mtoto mmoja kwa jina Naseeb Junior, baada ya kuachana na mwanamziki huyo wa Tanzania aliendelea na kuimba na kutoa nyimbo kathaa Pamoja na wimbo wa Sawa, Complicationship, Mood na mengineyo.

Mwingine ambaye amewai kua na mahusiano na Diamond ni Mwansocialaiti Zari Hassan kutoka nchi ya Uganda.

Zari aliyezaliwa tarehe 23 Septemba 1978 anayejulikana pia kama Zari the Boss Lady, ni mwanamuziki wa Uganda na mjasiriamali. Kwa sasa anaishi na anaendesha biashara yake kutoka Afrika Kusini.

Zari ana watoto wawili na Diamond wanaofahamika kama  Latiffah Dangote na Prince Riaz.

Baadhi ya nyimbo ambazo zari amewai kuzzimba ni Pamoja na Kikoona, Tolooba, Oliwange na meningenyo.