Akothee ajibu kuhusu kukosana na Zari Hassan, amtetea katika ugomvi na Fantana

"Nini kilichotokea kati yenu na Zari mlikuwa marafiki wakubwa, nakumbuka ukitusi juu yake?" aliulizwa.

Muhtasari

•Akothee alikabiliwa na swali tata kuhusu kile kilichotokea kati yake na aliyekuwa rafiki yake wa karibu, mwanasosholaiti Zari Hassan.

•Katika jibu lingine kwa shabiki, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alionekana kumtetea Zari kuhusu ugomvi wake na Fantana.

wakati wa urafiki wao
Akothee na Zari wakati wa urafiki wao
Image: HISANI

Siku ya Jumanne, mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee alikabiliwa na swali tata kuhusu kile kilichotokea kati yake na aliyekuwa rafiki yake wa karibu, mwanasosholaiti Zari Hassan.

Akothee alikuwa ametoa maoni yake kuhusu sehemu ya pili ya filamu ya Young, Famous and African iliyoachiwa hivi majuzi ambapo alimsifu mwanamitindo maarufu wa Nigeria Swanky Jerry kuhusu mitindo na ucheshi wake.

"Swanky. Usumbufu wa Young Famous African. @swankyjerry ndiye shoo yenyewe, huyu jamaa ananichekesha. Wakati anaingia, mazingira yanabadilika. Swanky ni yule Rafiki mmoja kwenye kikundi ambaye hutajua lini na jinsi ya kumzungumzia… Hisia zake za mitindo ! Ucheshi unahitaji kiwango fulani cha akili," Akothee alisema.

Mama huyo wa watoto watano aliweka wazi kwamba alikuwa akifuatilia filamu hiyo ya maisha halisi nchini Ufaransa.

Kama ilivyotarajiwa, mashabiki wake walikusanyika chini ya chapisho hilo kutoa maoni kuhusu chapisho hilo na wengine kuhusu kipindi hicho. Baadhi yao walionekana kumvutia rafiki yake wa karibu wa zamani, Zari.

Mtumiaji mmoja wa Instagram alimuuliza ni nini kiliendelea kati yake na mzazi mzenza huyo wa staa wa Bongo Diamond Platnumz.

"Tukiongea kuhusu Swanky Jerry, nini kilichotokea kati yenu na Zari mlikuwa marafiki wakubwa nakumbuka ukitusi juu yake?" shabiki alimuuliza.

Akothee alijibu, "Je! unataka kuanzisha kipindi kingine kando na netflix? Unataka kujua nini?

Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi kuhusiana  na swali la shabiki huyo.

Katika jibu lingine kwa shabiki, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alionekana kumtetea Zari kuhusu ugomvi wake na Fantana.

"Lakini Fantana alimfanyia Zari vibaya! Eish, kiboko yake yule!!" shabiki aliandika chini ya chapisho hilo.

Huku akionekana kumtetea mama huyo wa watoto watano, Akothee alisema, "Hapana, Fantana ni msichana mdogo asiye na heshima ambaye anahitaji kukua. Huwezi kushinda vita ya baby mama. Sikupenda, hakuna kiboko hapo."

Marafiki hao wa zamani walifunga pingu za maisha na wachumba wao mwezi uliopita. Akothee alitangulia kufanya harusi na Denis Shweizer mnamo Aprili 10 kabla ya Zari kufunga ndoa na Mganda Shakib Lutaaya siku chache baadaye.

Kulikuwa na madai kwamba Zari aliolewa kutokana na shinikizo baada ya rafikiye wa zamani kuolewa, madai aliyojitokeza kufutilia mbali.

"Kila kitu kiko mahali na ndio tulifanya Nikah. Na si kwa sababu ya shinikizo, sishindani na mtu yeyote. Sasa kwa sababu tu mtu katika nchi nyingine alifunga ndoa, watu hawapaswi kuolewa tena. Je, alikuwa wa kwanza kuolewa?” alisema.