logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa aelekea loji na sidechick, akutana na mkewe akitoka na mwanaume mwingine!

Je, tunaweza kusema 50/50 tu?

image
na Radio Jambo

Yanayojiri29 May 2023 - 12:51

Muhtasari


• Baadhi walimtaka mwanaume huyo naye kutoonesha hasira kwani alikuwa katika makosa sawa.

• Wengine walisema anapaswa kukasirika kwa sababu ni rahisi mwanaume kuoa wake wengi lakini si mke kuolewa na waume wengi.

Mwanaume na mke wasioelewana kwa ndoa

Kulikuwa na drama na timbwiri zito kwenye hoteli moja wakati mwanamume alifumaniana na mkewe katika hoteli na mwanamume mwingine ambapo pia yeye alikuwa na mpango wake wa kando.

Bila shaka, wanandoa hao, kila mmoja kwa wakati wake, walipata habari kwamba walikuwa wakidanganyana huku mume akimleta mpenzi wake hotelini kwake na kujua kwamba mke wake alikuwa akiburudika na mwanamume mwingine katika hoteli hiyo moja.

Mwanasheria kwa jina Bolanle Cole alichapisha matukio hayo ya kutokuwa mwaminifu kwenye tovuti Twitter.

Alidai kuwa mwanamume huyo alipoingia kwenye hoteli hiyo, alikutana na mke wake huku akitoka na mpenzi wake. Bolanle anadai kuwa mwenzake aliyemwandikia habari hizo alitamka kuwa mume amekasirika ilhali mwanamke hana wasiwasi.

Tweet hiyo ilisomeka; “Ni nini hasa kinatokea kwa watu wetu, uasherati umekitawala kizazi chetu. Rafiki wa wakili aliniambia hadithi hii sasa hivi kwamba, Mwanaume mmoja alimpeleka mpenzi wake hoteli moja mbali na ofisi yake na kukutana na mkewe akiwa na mwanamume mwingine wakati wanatoka hoteli moja 💔wakafumaniana uso kwa uso.”

“Je, tunaweza kusema 50/50 tu? Mwanaume ameumia sana, ana wazimu na hasira huku mwanamke hana wasiwasi wala hata kuonesha kujuta,🙃”

 

Tukio hilo lilivutia hisia mseto mitandaoni, baadhi wakimtaka mwanamume huyo pia kutoonesha hasira kwani naye alikuwa amekwenda kwenye hoteli hiyo kurina asali kutoka kwa mzinga usio wake, wakati kwa bahati mbaya au nzuri alikutana na mwanaume mwingine pia akijaribu kurina asali kutoka kwa mzinga wake.

“Sio 50-50, mwanaume anaweza kuoa wake 3 kwa wakati mmoja na kuishi katika nyumba moja, lakini mwanamke hawezi kuoa waume 2 kwa wakati mmoja.”

Wengine pia walisema wakajipata kwenye hali kama hiyo, anamwacha mpango wake wa kando na kumwendea mke wake na kumpa busu na kumtaka wasameheane na kupatiana nafasi za mwisho.

“Mimi, naenda tu kumuacha mpenzi wangu akimkumbatia mke wangu, "babe tusameheane, tujipe nafasi nyingine" mwingine alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved