logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Grand P adokeza kurudiana na mpenzi wake wa zamani Eudoxie

Mwimbaji wa Guinea Grand P amedokeza kurudiana na Eudoxie Yao.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 June 2023 - 07:33

Muhtasari


  • • Balozi huyo wa Guinea nchini Mali alikatisha mahusiano yake na mwanamitindo Yao mwaka wa 2021 baada ya kuwa kwenye mahusiano na mwanamitindo huyo kwa takriban miaka mitatu.
  • • Wawili hao walitangaza kukuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2020 baada ya kuchapisha picha wakiwa pamoja.
Balozi Grand P na mpenzi wake Eudoxie Yao.

Mwimbaji tajiri wa Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P amedokeza kurudiana na mwanamitindo kutoka Ivory Coast Eudoxie Yao.

Katika picha alizochapisha kwenye akaunti yake wawili hao wakipata chakula pamoja na ujumbe kuwa mapenzi hayaishi.

“True Love never ends” aliandika Grand P kwenye picha aliyoweka kwenye Facebook.

Mashabiki wa mwanamziki huyo mwenye umbile la mbilikimo waliwasherehekea kurudiana kwao.

Aprili mwaka huu Grand P alitangaza kuingia katika uhusiano na mwanadada mwingine   mwenye asili ya Kiasia, Yubai Zhang.

Grand P alitangaza mahusiano yao kupitia akaunti yake ya Facebook akithibitisha mapenzi yake na mrembo huyo wa Kiasia na kuweka wazi kuwa hakuna nafasi ya watu wenye wivu maishani mwao.

"Yubai Zhang wangu, hakuna nafasi kwa watu wenye wivu," alisema chini ya picha zake na Zhang alizochapisha Facebook.

Balozi huyo wa Guinea nchini Mali alikatisha mahusiano yake na mwanamitindo Yao mwaka wa 2021 baada ya kuwa kwenye mahusiano na mwanamitindo huyo kwa takriban miaka mitatu.

Wawili hao walitangaza kukuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2020 baada ya kuchapisha picha wakiwa pamoja.

Mahusiano hayo yaliibua gumzo mitandaoni kwa ajili ya uzani wao, mashabiki walishangaa ni vipi Grand P mweye mwili mdogo anaweza kuwa kwenye mahusiano na mwanamke huyo aliyeonekana kumzidi  kwa uzani kwa kiasi kikubwa.

Lakini licha ya wafuasi wao wengi kutokubaliani na chaguo la Grand P la kuchumbiana na Yao, wawili hao walisisitiza kuwa wana furaha na wataendelea kuwa kwenye mahusiano.

"Tuna Furaha tukiwa pamoja, na hicho ndicho kitu cha maana. Asante kwa kila mmoja wenu kwa msaada wenu, ya kimwili haihesabiki katika mahusiano” aliandika Yao katika akaunti yake ya Instagram.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved