Mshtuko baada ya warembo kujitokeza wakidai wana mimba ya mwimbaji Davido

Anita Brown alidai kuwa Davido alimpa pesa ili kuitoa mimba hiyo, lakini alikataa.

Muhtasari

•Anita alifichua gumzo yake na mwimbaji huyo wa Afrobeats kwa madai kuwa amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi naye na hata anatarajia mtoto naye.

•Kupitia mtandaoni, Ivanna alibainisha kuwa hakujua kuwa sio yeye pekee ambaye mwimbaji huyo alitunga ujauzito.

Davido
Image: HISANI

Mwanamke wa pili amejitokeza na kudai kuwa yeye pia ana mimba ya mwimbaji wa Nigeria David Adedeji Adeleke almaarufu Davido katika muda wa siku mbili tu.

Siku ya Jumatano, mrembo wa Marekani, Anita Brown almaarufu Ninatheelite alifichua gumzo yake na mwimbaji huyo wa Afrobeats kwa madai kuwa amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi naye na hata anatarajia mtoto naye.

Anita alidai alikutana na mwimbaji huyo mwaka wa 2017, wakiwa safarini Dubai na wawili hao wakawa kwenye uhusiano wa mbali hadi 2020 wakati janga la Corona lilitokea.

“Kinachoniuwa sana ni simulizi hii ya wanaume waliolewa ambayo nyinyi nyote mnaiburuza, oh najihusisha na mwanamume aliyeoa, acheni, hapana sikujua kuwa ameolewa haki ya Mungu, sikujua kama ameolewa, nenda kwenye ukurasa wake , je inaonekana kama ameoa ama nimechanganyikiwa?,” Anita aliwaambia watu waliokuwa wakimshutumu kwa kuchumbiana na mwanamume aliyeoa.

Katika screenshot za yanayodaiwa kuwa mazungumzo yao ambayo Anita alichapisha, Davido alionekana akimsihi asimwambie mtu yeyote kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wake ambaye hajazaliwa.

Pia alidai kuwa Davido alimpa pesa ili kuitoa mimba hiyo, lakini alikataa.

“Sikuwa na hamu ya kuolewa hivi sasa. Niligundua baadaye kwamba mimi ni mjamzito, kwa hivyo mko mbali," Anita alisema.

Saa chache tu baada ya Anita Brown kujitokeza, mwanamke wa Ufaransa, Ivanna Bay alijitokeza pia kudai kuwa ana ujauzito wa mtoto wa Davido.

Kupitia mtandaoni, Ivanna alibainisha kuwa hakujua kuwa sio yeye pekee ambaye mwimbaji huyo alitunga ujauzito.

"Niliamka asubuhi na kuona kwamba sio mimi pekee mwanamke ambaye David alipata ujauzito. Nimesikitishwa sana na mtu wa aina hii. Wanawake, kuweni makini. Bado nina mimba. Kwa hivyo tuonane chini ya miezi 9 sasa,” Ivanna aliandika.

Aliendelea, "Kwa hivyo niambieni, uko na baby mama wangapi, je, tunapaswa kuwa tayari kwa timu ya soka?"