Threads: MrBeast ni wa kwanza kufikia wafuasi Milioni 1

MrBeast aliongeza kwa mzaha, "Ninahisi kama ninacheat kwenye Twitter kwa kutumia programu hii."

Muhtasari

• MrBeast amejitangaza kwa fahari kuwa Mkurugenzi mkuu wa Future Threads kwenye wasifu wake, na maudhui yake ya kuvutia yalipata wafuasi milioni baada ya kuchapisha mara tatu pekee.

• Guinness World Records iliripoti kwamba ingawa akaunti zingine zilifikia nambari hii hapo awali, zilikuwa za mashirika kama Instagram na National Geographic, na kumfanya MrBeast kuwa wa kwanza kupata ufuasi mkubwa kama huo.

MrBeast aweka rekodi kama mtu wa kwanza kufikia wafuasi milioni 1
MrBeast aweka rekodi kama mtu wa kwanza kufikia wafuasi milioni 1
Image: Instagram

MwanaYouTube maarufu MrBeast, anayejulikana pia kama Jimmy Donaldson, amekuwa mtu wa kwanza kufikisha wafuasi milioni 1 kwenye mtandao mpya wa kijamii wa Threads.

MrBeast amejitangaza kwa fahari kuwa Mkurugenzi mkuu wa Future Threads kwenye wasifu wake, na maudhui yake ya kuvutia yalipata wafuasi milioni baada ya kuchapisha mara tatu pekee.

MrBeast aliafikia hatua hii muhimu saa 8:42 mchana, tarehe 6 Julai.

Alipogundua mafanikio yake ya kuvunja rekodi, aliandika kwenye Twitter, "Shhhh, msiruhusu polisi wa Twitter kujua ninawacheat."

Threads ambayo inakisiwa kuipa Twitter upinzani mkali ilizinduliwa Julai 5, na ilimchukua MrBeast muda wa saa moja kupata halaiki ya wafuasi.

Guinness World Records iliripoti kwamba ingawa akaunti zingine zilifikia nambari hii hapo awali, zilikuwa za mashirika kama Instagram na National Geographic, na kumfanya MrBeast kuwa wa kwanza kupata ufuasi mkubwa kama huo.

Katika chapisho lake la kwanza muda mfupi baada ya programu kuanza kutumika MrBeast aliuliza, "Soooooo, ni muda gani hadi sisi pia tuwe waraibu wa programu hii? Lol."

Pia aliwashirikisha mashabiki wake kwa kuwaalika kupenda chapisho ikiwa waliamini Mark Zuckerberg, Mkurugenzi Mkuu wa Meta, anafaa kumteua kama Mkurugenzi Mkuu wa Threads.

MrBeast aliongeza kwa mzaha, "Ninahisi kama ninacheat kwenye Twitter kwa kutumia programu hii."

Ana wafuasi milioni 38.5 kwenye Instagram na wafuasi milioni 165 kwenye YouTube.

Zaidi ya hayo, ana mataji kadhaa ya Rekodi za Dunia za Guinness, kama vile mtu aliyeingiza mapato mengi zaidi kwenye YouTube mwaka wa 2021, aliyeripotiwa kupokea shilingi 54,000,000 na mwanamume mmoja aliye na wafuasi wengi kwenye YouTube.