Uume huacha kukua mtu akiwa na umri wa miaka 21, hakuna dawa ya kurefusha - Daktari

"Watu au makampuni yanayotangaza dawa na michanganyiko wanayodai yana uwezo wa kurefusha uume au kuufanya kuwa mrefu zaidi wanadanganya tu wanaume wasiojiamini." - Daktari.

Muhtasari

• "Uume huacha kukua ukiwa na umri wa miaka 21, hakuna dawa, mazoezi yanaweza kuufanya kuwa mkubwa au mrefu zaidi" - Daktari

Mwanaume afariki kwa kudungwa sindano ya kuongeza uume.
Mwanaume afariki kwa kudungwa sindano ya kuongeza uume.
Image: BBC PIDGIN

Daktari mmoja anayeishi nchini Uingereza kupitia mtandao wa Twitter ametoa ushauri wa kimatibabu kwa vijana wanaohaha kutaka kurefusha na kunenepesha uume wao.

Kwa mujibu wa daktari huyo kwa jina Dr Olufunmilayo Ogunsanya, raia wa Nigeria anayefanya shughuli zake nchini Uingereza, wanaume wanafaa kutosheka na kuridhika na urefu na unene wa sehemu zao za siri pindi wanapopita umri wa miaka 21.

Daktari huyo anahoji kwamba kila mvulana uume wake unafika ukomo wa kukua anapofikisha umri wa miaka 21, Zaidi ya hapo hakuna dawa au mazoezi yoyote yanayoweza kuufanya uwe mkubwa wala kuwa mrefu.

Kulingana na daktari na mshawishi wa Twitter ambaye ni maarufu kwa jina la Dk. Olufunmilayo, akiwa na umri wa miaka 21, sehemu za siri za kiume huacha kukua na jaribio lolote la kubadilika halina tija.

Aliongeza kuwa watu au makampuni yanayotangaza dawa na michanganyiko wanayodai yana uwezo wa kurefusha uume au kuufanya kuwa mrefu zaidi wanadanganya tu wanaume wasiojiamini.

"HAKUNA ushahidi wa kisayansi uliothibitishwa kuwa cream au dawa yoyote inaweza kuongeza uume kwa kiasi kikubwa. Au hata kuongeza kabisa. YOTE ni ulaghai. Na udanganyifu. Wanaume kwenye mabango yao tayari ni wanamitindo wamejaaliwa sana ambao uume wao ulikua ASILI. Na ndivyo hivyo,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

uume
uume

Dkt Olufunmilayo alienda mbali zaidi kuwaonya wanaume dhidi ya uwezekano wa kufa kabla ya wakati au kupata matokeo ya kudhoofisha huku wakijaribu bila matunda kuongeza ukubwa na urefu wa uanaume wao.

"Baadhi ya wanaume wanafikiri kujichua mara kwa mara au mitindo fulani ya ngono itaongeza au kurefusha uume. Ndugu yangu, usife kabla ya wakati wako. Ulichonacho sasa hivi ni YOTE utakachokuwa nacho. Tumia nguvu zako kuutumia ipasavyo, badala ya kupoteza pesa kununua uwongo,” alionya.

uume
uume

Hata hivyo, kuna wengine wanahoji kwamba ukubwa au urefu wa uume hauzingatiwi sana wakati wat endo la kujamiiana bali cha muhimu ni ustadi na weledi wa mhusika katika kumridhisha mwenza wake.