Mwanamume ukitaka kuishi miaka mingi oa wanawake wengi - Pasta mtata ashauri

Alieleza kuwa ndoa ya mke mmoja ni utamaduni wa Kimagharibi huku akisisitiza kuwa mitala ni sehemu ya utamaduni wa Afrika.

Muhtasari

• Ndoa ya mke mmoja iliyowekwa kijamii ilianzishwa kwanza katika Ugiriki na Roma ya kale, kulingana na Feeld.

Mchungaji Meshack Aboh
Mchungaji Meshack Aboh
Image: Screengrab//TIKTOK

Mchungaji mmoja mweney utata mwingi nchini Ghana Meshack Aboh amewapa wanaume siri kubwa iwapo wana azma ya kuishi miaka mingi duniani.

Mchungaji huyo katika kipindi cha uchambuzi wa Biblia kwenye runinga ya UTV nchini humo Jumamosi iliyopita, alitoa ushauri wenye utata, akiwaambia wanaume kwamba siri ya kuishi miaka mingi ni kuoa wanawake wengi vile vile.

Mchungaji Aboh, ambaye pia yeye ana wanawake Zaidi ya mmoja na haogopi hadharani kupigia debe ndoa ya mitala alisema kuwa watu haswa Wakristo hawafai kuogopa wala kujiona kama wanatenda dhambi linalokuja wazo la kuongeza mke mwingine.

Alieleza kuwa ndoa ya mke mmoja ni utamaduni wa Kimagharibi huku akisisitiza kuwa mitala ni sehemu ya utamaduni wa Afrika.

"Ikiwa unataka kuishi muda mrefu, oa wanawake wengi," Mchungaji Aboh alisema.

Mhubiri huyo, ambaye alifichua kwamba ana wake wawili, alitumia maisha yake kuthibitisha kwamba ndoa za wake wengi zinaweza kuwa na usawa.

Ndoa ya mke mmoja iliyowekwa kijamii ilianzishwa kwanza katika Ugiriki na Roma ya kale, kulingana na Feeld.

Tazama hii hapa video ya mchungaji huyo akitoa ushauri huo huku pia akitetea vikali msimamo wake ambao unachukuliwa kuwa ni wa kupotosha katika malimwengu ya Ukristo.