logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kamene Goro afunguka kuhusu kuwa na mimba ya mtoto wake wa kwanza

Kamene alilazimika kuweka mambo wazi baada ya baadhi ya wanamitandao wa Kenya kudai kuwa ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri30 August 2023 - 07:15

Muhtasari


•Kamene alilazimika kuweka mambo wazi baada ya baadhi ya wanamitandao wa Kenya kudai kuwa ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.

•Kamene aliweka wazi kuwa yeye si mjamzito na kubainisha kuwa kama angekuwa, hangeona haya kudhihirishia walimwengu.

Jumatano asubuhi, aliyekuwa mtangazaji wa radio Kamene Goro alilazimika kuweka mambo wazi baada ya baadhi ya wanamitandao wa Kenya kudai kuwa ana ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.

Kwenye sehemu ya maoni ya moja ya chapisho la mwanahabari huyo, baadhi ya Wakenya walionekana kuwa na maneno mbalimbali ya kusema kuhusu mwili wake huku baadhi yao wakidai kuwa unaonekana mkubwa kuliko kawaida.

Katika majibu yake, mke huyo wa Deejay Bonez alisema kuwa maoni hayo yalimshtua na kusema anashindwa kuelewa kwa nini watu wanaona ni sawa kuwa na chuki  na kukisia mambo kuhusu maisha yake.

"Kwa hivyo niliamka Asubuhi hii kwa rundo zima la maoni ya chuki, ya ujinga kwenye chapisho langu la mwisho, na nimecheka na kushangazwa. Sitawahi kuelewa ni jinsi gani ni silika ya kwanza ya mtu kuwa na chuki au ubaya na mawazo mabaya ambayo baadhi yenu wanataka kuweka juu ya maisha YANGU. Inanishtua na kunishangaza,” Kamene alisema kupitia mtandao wa Instagram.

Mwanahabari huyo mwenye umri wa miaka 31 aliweka wazi kuwa yeye si mjamzito na kubainisha kuwa kama angekuwa, hangeona haya kudhihirishia walimwengu.

“Mimi si mjamzito, kama ningekuwa na imani dunia nzima ingejua tangu siku ya kwanza, si kwamba nahitaji kueleza hilo, na ninaupenda mwili wangu kwa mikunjo na kingo zake, sina deni kwa mtu aina ya mwili unaotaka au. tarajia nipate, tuyaweke sawa,” alisema.

Aliongeza, “Babygirl ako tu sawa, kuishi maisha ambayo nimekuwa nikitamani kuishi,  asubuhi hii si uanze kuishi maisha ya aina unayotaka kuishi na uache kuishi na hiyo chuki ndani yako, utaanza kuchapa.

Hivi majuzi, wakati wa mazungumzo ya wazi na mashabiki wake kwenye kipindi cha Maswali na Majibu kwenye Instagram, Kamene alifichua kwamba  watu watasubiri  sana ikiwa wanatarajia kumuona akipata mimba.

Wakati wa kipindi hicho siku chache zilizopita, swali liliibuka kuhusu mipango ya yeye na Deejay Bonez wa kupanua familia yao.

Shabiki mmoja aliyekuwa na hamu ya kutaka kujua aliuliza, "Tungoje mtoto hadi lini?"

Kamene alijibu kwa jibu fupi lakini lenye kueleweka, "Mtangoja" .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved