Samidoh ajibu kwa ukali mwingi baada ya kuagizwa awatembelee watoto wake Marekani

Watoto watatu wa mwimbaji huyo wamekuwa Marekani na mama yao Edday Nderitu katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.

Muhtasari

•Mtumiaji mmoja wa Facebook aliyejitambulisha kama Teresiah Nyambura Wainaina alimtaka mwimbaji huyo kupitia mahali watoto wake walipo.

•Katika majibu yake, mwimbaji Mugithi alidokeza kuwa hakumbuki akizaa na mwanamtandao huyo.

Image: FACEBOOK.

Mwimbaji maarufu wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh alijibu kwa ukali baada ya shabiki kumuagiza awatembelee watoto wake Marekani.

Samidoh ambaye kwa sasa yuko kwenye ziara ya muziki jijini Melbourne, Australia alikuwa amechapisha picha yake akiwa mjini humo na kushiriki nukuu ya kusisimua.

"Katika vita kati ya moyo na ubongo, mimi husikiliza tumbo langu kila wakati," aliandika.

Kama kawaida, wanamitandao walikusanyika chini ya chapisho hilo na kutoa majibu ya kila aina huku wengine wakionekana kumshambulia baba huyo wa watoto watano.

Mtumiaji mmoja wa Facebook aliyejitambulisha kama Teresiah Nyambura Wainaina alimtaka mwimbaji huyo kupitia mahali watoto wake walipo.

"Na upitie watoto boss," aliandika.

Katika majibu yake, mwimbaji Mugithi alidokeza kuwa hakumbuki akizaa na mwanamtandao huyo.

Alijibu, “Hehe, nakumbuka nikizaa nawe kweli nyakanga bibi wa Hoji.”

Mwanamtandao mwingine alijaribu kumuuliza msanii huyo kama yuko sawa akidai kuwa watoto wake ambao wako na mama yao huko USA wanakaribia kuanza shule.

"Father Abraham, watoto wako na Nothing but prayers ni kama walijoin shule huko USA.. I hope uko sawa," shabiki aliandika.

Samidoh alijibu, “Siko sawa mpaka u deworm.”

Watoto watatu wa mwanamuziki huyo wamekuwa Marekani na mama yao Edday Nderitu katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.

Mwezi uliopita, Edday aliweka wazi kuwa alimuacha mumewe Samidoh ili kuwa na mwanamke ambaye alionekana kumtaka zaidi.

"Wacha nifafanue mambo machache ambayo yalishirikiwa mtandaoni na sio sahihi. Siko kwenye ndoa ya wake wengi, kama ilivyoelezwa nilimuacha mume kwa yeyote aliyemhitaji zaidi,” Edday alisema kupitia Facebook.

Aliongeza, "Nilifanya uamuzi wa kujiondoa mimi na watoto wangu kutoka kwa mazingira hayo yenye sumu, haswa binti yangu kijana ambaye kwa bahati mbaya anapokea moja kwa moja tabia isiyoaminika iliyoonyeshwa."

Mama huyo wa watoto watatu alidokeza kuwa hajutii uamuzi wa kugura ndoa yake ya miaka mingi na akaweka wazi kuwa ameweza kuwalea watoto wake bila usaidizi wowote.

Pia alizungumzia madai ya Karen Nyamu kwamba yeye na watoto wake huwa wanawasiliana na mwimbaji Mugithi kwa simu.

"Kuhusu mawasiliano na simu za video, nitaachia hapo kwani baadhi ya watu wanaonekana kuwepo wakati hilo linafanyika lakini mimi sifahamu. Katika msimu huu mpya wa maisha yangu, sihitaji drama yoyote, nahitaji amani tu, natumai kipindi kijacho cha mfululizo huu jina langu litaachwa,” alisema.