logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Tupa mistari!" Vera Sidika aruhusu maombi ya kuwa mpenzi wake baada ya kuachana na Mauzo

Jumatano, mwanamuziki Brown Mauzo alitangaza kuwa wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

image
na Samuel Maina

Burudani31 August 2023 - 06:28

Muhtasari


  • •Vera alitoa dokezo hilo alipokuwa akimjibu rapa wa Kenya, Breeder LW kwenye chapisho lake la Instagram siku ya Jumatano.
  • •Vera alimshauri Breeder ajaribu bahati yake na kudokeza kwamba baada ya kufanya hivyo angejaribiwa kwa nafasi hiyo ya mpenzi wake.

Mwanasosholaiti Vera Sidika amedokeza kuwa yuko tayari kutathmini maombi ya watu wanaomtaka baada ya kutengana na mwimbaji Brown Mauzo.

Mama huyo wa watoto wawili alitoa dokezo hilo alipokuwa akimjibu rapa wa Kenya, Breeder LW kwenye chapisho lake la Instagram siku ya Jumatano.

Rapa huyo alimtania Vera akimuuliza kama yuko tayari kujaribu kuchumbiana kufuatia habari za kutengana kwake na mzazi mwenzake.

“Naskia upo single, unaweza kumingle??" Breeder alimuuliza Vera.

Katika majibu yake, mwanasosholaiti huyo alimshauri Breeder ajaribu bahati yake na kudokeza kwamba baada ya kufanya hivyo angejaribiwa kwa nafasi hiyo ya mpenzi wake.

"Shoot your shot, kuna vetting," alisema.

Kumaanisha: Tupa mistari yako, kuna ukaguzi.

Jumatano, mwanamuziki Brown Mauzo alitangaza kuwa wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Mauzo aliendelea kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"

Mauzo alidokeza kuwa ukurasa  unaofuata wa maisha yao utakuwa kuhsu uponyaji wa moyo baada ya kuachana na kukumbatia yake yaliyo mbele.

"Ingawa sehemu zetu zinaweza kutofautiana, tutathamini kumbukumbu ambazo tumeunda pamoja. Sote tunasalia kushukuru kwa masomo tuliyojifunza na ukuzi ambao tumepitia. Lengo letu sasa ni uponyaji na kukumbatia siku zijazo kwa mioyo iliyo wazi. Asanteni kwa mara nyingine tena kwa kuwa sehemu ya safari yetu,” alisema.

Saa moja baadaye, Vera alishiriki picha zake akiwa ndani ya ndege inayoelekea mahali ambapo aliwaacha mashabiki wake wakisie tu.

Katika picha hizo, mama huyo wa watoto wawili alionekana kutosumbuliwa wala kutikiswa na chochote alipokuwa amejistarehesha kwenye sehemu ya kifahari ya ndege.

"Catch flights, not feelings, Guess my next stop," Vera alisema na kuandamana na ujumbe wake wenye emoji ya ndege inayosonga.

Kumaanisha: Chukua safari za ndege, sio hisia, Kisia nitakakosiamama tena.

Vera na Mauzo wamekuwa pamoja kwa takriban miaka mitatu na tayari wawili hao wana watoto wawili pamoja, mvulana na msichana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved