logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vera Sidika, Brown Mauzo wachocheana wivu baada ya kuachana, waweka wazi wako sokoni

“Mmesema ni Masaa ya kurudi soko.. tutaoga baadaye," Vera alisema.

image
na Samuel Maina

Burudani01 September 2023 - 05:37

Muhtasari


  • •Vera ambaye kwa sasa yuko Marekani alichapisha picha na video za kuvutia na kujigamba jinsi alivyo na uwezo wa kushinda wanaume.
  • •Mauzo pia alidokeza kuwa yuko tayari kujaribu mapenzi mara moja tena baada ya kutengana na mama huyo wa watoto wake wawili.

Mwanasosholaiti wa Kenya Vera Sidika na mzazi mwenzake Brown Mauzo wote wamedokeza kuwa wako tayari kwa hatua ya maisha yao inayofuata baada ya kuachana.

Wapenzi hao wa zamani ambao wana watoto wawili pamoja wameonyesha kuwa wako tayari kujaribu mahusiano mapya kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii.

Siku ya Alhamisi, Vera ambaye kwa sasa yuko Marekani alichapisha picha na video za kuvutia na kujigamba jinsi alivyo na uwezo wa kushinda wanaume.

"Siwezi kugeuza maji kuwa divai lakini ninaweza kumgeuza Baby Daddy wako kuwa wangu," Vera aliandika chini ya picha zake maridadi.

Katika chapisho lingine, aliweka video ikionyesha mwili wake mzuri na katika sehemu ya maelezo akasema, “Mmesema ni Masaa ya kurudi soko.. tutaoga baadaye.

Jumatano jioni, Vera  alidokeza kuwa yuko tayari kutathmini maombi ya watu wanaomtaka baada ya kutengana na mumewe.

Mwanasosholaiti huyo alitoa dokezo hilo alipokuwa akimjibu rapa Breeder LW kwenye chapisho lake la Instagram.

Rapa huyo alimtania Vera akimuuliza kama yuko tayari kujaribu kuchumbiana kufuatia habari za kutengana kwake na mzazi mwenzake.

“Naskia upo single, unaweza kumingle??" Breeder alimuuliza Vera.

Katika majibu yake, mwanasosholaiti huyo alimshauri Breeder ajaribu bahati yake na kudokeza kwamba baada ya kufanya hivyo angejaribiwa kwa nafasi hiyo ya mpenzi wake.

"Shoot your shot, kuna vetting," alisema.

Kumaanisha: Tupa mistari yako, kuna ukaguzi.

Pia alifichua kuwa ameweza kupokea jumbe nyingi sana baada ya mzazi mwenzake Brown Mauzo kutangaza kuachana kwao siku ya Jumatano.

Jumatano jioni, Mauzo pia alidokeza kuwa yuko tayari kujaribu mapenzi mara moja tena baada ya kutengana na mama huyo wa watoto wake wawili.

“Brown, unataka kupenda tena? Hakika, leo, leo kesho, sasa. Upendo hukujia,” Mauzo aliandika.

Katika chapisho lingine, mwimbaji huyo alishiriki meme akidokeza kuwa kuna wanawake wengi wanamfuata nyuma tangu ‘arudi sokoni.

Siku mbili zilizopita, Mauzo alitangaza kuwa wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Mauzo aliendelea kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"

Mauzo alidokeza kuwa ukurasa  unaofuata wa maisha yao utakuwa kuhsu uponyaji wa moyo baada ya kuachana na kukumbatia yake yaliyo mbele.

"Ingawa sehemu zetu zinaweza kutofautiana, tutathamini kumbukumbu ambazo tumeunda pamoja. Sote tunasalia kushukuru kwa masomo tuliyojifunza na ukuzi ambao tumepitia. Lengo letu sasa ni uponyaji na kukumbatia siku zijazo kwa mioyo iliyo wazi. Asanteni kwa mara nyingine tena kwa kuwa sehemu ya safari yetu,” alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved