Warembo wafurika kanisani wakivalia mavazi ya harusi kuomba Mungu kuwapa wanaume - video

"Wanawake walioko katika miaka yao ya 20 wanacheka kwenye maoni, subiri hadi 30-33 ujue kusema mambo haya halisi. Naomba Mungu awajibu.” mmoja alisema.

Muhtasari

"Ni lini ndoa ikawa lazima. Ni wakati muafaka kwa wanawake kuelewa hilo, kutoolewa hakukufanyi wewe kuwa mwanamke.” mmoja aliuliza.

Harusi
Harusi
Image: TikTok

Video moja ikiwaonesha makumi ya kina dada ambao wanatafuta wanaume wa kuwaona imeenezwa mitandaoni, haswa baada ya kubainika kwamba walifurika kanisani wakiwa na mavazi ya bibi harusi ili kuomba Mungu kuwabariki na harusi.

Katika video hiyo iliyosambaa mitandaoni, umati wa wanawake wa rika tofauti nchini walivamia kanisa lao wakiwa wamevalia mavazi ya harusi.

Kina dada hao wengi ambao wote walivalia nadhifu mavazi meupe ya bibi harusi walionekana kajisani walisali kwa maombi ya kila aina katika kile kilichoonekana kama ni mkusanyiko wa waumini wanaofanya maombi kwa ndimi za Roho mtakatifu – wakiomba Mungu kutuma wanaume wa kuwaona kwao ili kukutana nao baada ya maombi.

Licha ya kwamba dunia ya sasa, wanawake wengi wameonekana kusonga mbali na dhana ya kwamba kuolewa ndio njia pekee ya mwanamke kuheshimika katika jamii, wanawake hao walionekana kuwa na ari na uchu wa kutaka kubadilisha hali yao ya kindoa kwa kupata mtu wa kuitwa kwa jina lake kwamba huyu ni mke wa mwaflani.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya kufurahisha tuliyokusanya kutoka kwa chapisho hilo la TikTok;

@Malkia! alisema: "Wanawake walioko katika miaka yao ya 20 wanacheka kwenye maoni, subiri hadi 30-33 ujue kusema mambo haya halisi. Naomba Mungu awajibu.”

@Yin ​​Divom alishangaa: "Ni lini ndoa ikawa lazima. Ni wakati muafaka kwa wanawake kuelewa hilo, kutoolewa hakukufanyi wewe kuwa mwanamke.”

@Prosy alisema: “Hao waache utani wakuwe serious. ndoa ni kama kiota/zimba …ndege ndani ya ngome anatafuta njia ya kutoka, lakini wale wanaoruka huku na huku wanatafuta tu ngome?”

Maoni yako ni yapi?