logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Onyo kali ambalo mume wa Nyota Ndogo amempa baada ya kushika mimba ya mtoto wao

Nyota Ndogo aliweka wazi kuwa amepigwa marufuku kuzungumza kuhusu ujauzito wake na vyombo vya habari au mamlaka

image
na SAMUEL MAINA

Burudani08 September 2023 - 05:43

Muhtasari


  • •Nyota Ndogo aliweka wazi kuwa amepigwa marufuku kuzungumza kuhusu ujauzito wake na vyombo vya habari au mamlaka na mume wake mzungu, Henning Neilsen.
  • •Pia alieleza sababu ya ukimya wake katika siku za hivi majuzi akidokeza kwamba amekuwa na shughuli nyingi tu kazini.

Mwimbaji mkongwe mzaliwa wa Pwani, Mwanaisha Abdalla kwa almaarufu Nyota Ndogo amewashukuru wale wote waliompongeza kufuatia taarifa za hivi punde za ujauzito wake.

Katika taarifa yake siku ya  Alhamisi jioni, mama huyo wa watoto wawili hata hivyo aliweka wazi kuwa amepigwa marufuku kuzungumza kuhusu ujauzito wake na vyombo vya habari au mamlaka na mume wake mzungu, Henning Neilsen.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 42 alisema ameruhusiwa tu kujizungumzia yeye na muziki wake na sio ujauzito hadi atakapojifungua.

“Asanteni kwa hongera zenu, lakini media mtanisamehe mume wangu amesema hataki kuona kwenye kituo chochote cha radio TV ama polisi nikiongelea hali yangu. Kwa hiyo endapo nitatoa interview iwe ya mimi na mziki wangu na sio ujauzito wangu, ama nisitoe mpaka nijifungue,” Nyota Ndogo alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mwanamuziki huyo ambaye sasa anaendesha mkahawa katika eneo la Voi aliambatanisha taarifa yake na video inayomuonyesha akinengua mauno huku wimbo wa kumshukuru Mungu ukicheza. Katika video hiyo, tumbo lake lilionekana kuchomoza sana, thibitisho kwamba kwa kweli amebeba ujauzito wa mtoto wake wa tatu.

Katika taarifa yake, pia alieleza sababu ya ukimya wake katika siku za hivi majuzi akidokeza kwamba amekuwa na shughuli nyingi tu kazini.

“Samahanini sana nimekuwa kimya, nikwambie kazini kuleee kwa machapati, maharage pilau. Mpishi wangu ameenda mapumziko kwa hiyo saaa kumi na moja alfajiri nafaa kufika kazini,” alisema.

Nyota Ndogo alitangaza habari za ujauzito wake siku ya Jumanne kutumia picha ambayo  ilimuonyesha akiwa ameshikilia tumbo lake lililochomoza.Hata hivyo, hakufichua maelezo yoyote zaidi katika sehemu ya maelezo na aliwaacha mashabiki kukisia tu.

Licha ya hayo, wanamitandao ambao walitoa maoni chini ya chapisho lake, wakiwemo watu mashuhuri wenzake walionekana kushawishika kuwa kweli ni mjamzito huku wengi wao wakichukua hatua zaidi ya kumpongeza.

Tazama baadhi ya maoni;

Wahukagwi: Hongera sana mpenzi wangu.

Lill_fii: Hongera sana

Millychebby: Hongera

Fatma_unbreakable: Ma Sha Allah hongera sana

celestinegachuhi: Hongera

Nyota Ndogo tayari ni mama wa watoto wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike, ambao alipata na aliyekuwa mume wake. Kwa sasa yuko kwenye ndoa rasmi na mwanaume mzungu kutoka Denmark, Bw Henning Neilsen.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved