Wakristo igeni mfano wa waislamu, Pasta Ezekiel ashauri

"Kuweni kama waislamu kwa msikiti hakuna cheo," Pasta Ezekiel aliwaambia washirika wake.

Muhtasari

• Wakristo hawana masaa ya kuomba pasta Ezekiel wa Kanisa la new life asema.

Mchungaji Ezekiel Odero.
Mchungaji Ezekiel Odero.
Image: MAKTABA

Muhubiri wa kanisa la Newlife Prayer Center lililoko Mavueni Kaunti  ya Kilifi Ezekiel Odero kwenye ibada na washirika wake  amewashauri Wakristo kuchukua mfano wa waislamu.

"Kuweni kama waislamu kwa msikiti hakuna cheo," Pasta  Ezekiel aliwaambia washirika wake.

"Ukienda kwa msikiti utapata watu wote wakipiga magoti  kwa heshima ya mungu wao mdogo kwa mkubwa hakuna cheo," aliongeza.

Kiongozi huyo wa kanisa aliwapea mfano jinsi na ambavyo waislamu ikifika ni wakati wao wa kuomba hata kama wako katika Benki hufunga milango yote kwa heshima na kukimbia msikitini.

Ezekiel alisema kuwa wakristo wanaficha imani yao huku akisema kuwa huwezi pata mkristo anaomba hadharani na hata kama anaomba atakuwa anaficha .

Katika ibada hiyo Pasta huyu aliwaomba viongozi wa kanisa za wakristo kufanya kazi wakiogopa Mungu huku akisema kuwa wengi si mfano mzuri kwa kanisa akitoa mfano jinsi viongozi hawa wanapenda kutembea na vipakatalishi vyao vikiwa wazi lakini Bibilia huficha wasionekane nayo hadharani.

"Mumeacha mungu wenu mnavaa mavazi na ambayo hayana heshima na viongozi wenu wanakataa kuwaambia kwa maana wanadhani wakiwakashifu watatoka na kuacha kuwa washirika."

"Wengi wenu hampati masaa ya kuomba kwa maana mko na saa na biashara zenu na ambazo zinazidi kufilisika kuweni kama waislamu ikifika ni saa ya kuomba wao hufunga na kwenda kwa msikiti na kuomba na biashara zao ndio zinanawiri," Ezekiel aliwaambia washirika wake kwenye ibada.