logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pongezi ya vesha Okello baada ya Akothee kupata dili nono

Mwanamuziki maarufu Akothee apata  nafasi ya kuwa balozi wa mauzo

image
na

Makala14 September 2023 - 08:13

Muhtasari


•Vesha Okello binti ya Akothee amupongeza kwa kuwa balozi wa mauzo katika kumpuni ya ndege

Binti ya mwanamuziki maarufu nchini kenya Akothee ,amemsifu sana kwa dili nono ambayo alipata.

Vesha Okello na ambaye ni mmoja kati ya mabinti wa Akothee amemutaja mamake Akothee baada kutunukiwa dili nono na kampuni ya uchukuzi wa  ndege Skyward express kuwa balozi wa mauzo.

"Niruhusu leo nijisifu kidogo jamani mama yangu ni Akothee,mwanamke wa Alpha, hodari na thamani kubwa na zaidi ya yote ni mchapakazi  ,niko na wewe nyakati zote madam impact!!pokea maua yako mama najivunia na wewe"alisema vesha katika mtandao wake wa instagram.

Kampuni ya skyward expres imemtunuku Akothe kuwa balozi wa mauzo kwenye usafiri wao na ambao ulianza kutoka Nairobi hadi Migori.

Kwenye kanda ya video msanii na mwanamuziki Akothee alionekana akipeperusha bendera katika mojawapo ya ndege ya Skyward express baada ya kupewa jukumu la kuwa balozi wa mauzo.

Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen pamoja na mama Ida Odinga walikuwa wageni wakuu kwenye sherehe ya ufunguzi wa safari za kaunti ya migori kupitia usafiri wa dege

viongozi wakishirikia na Akothee walishabikia sana kampuni hii kwa usafiri huu na ambao wengi walisema kuwa utarahisha uchukuzi katika kuanti ya migori

Baadhi ya wasafiri walipata nafasi ya kusafiri kwa dege hii kwa mara ya kwanza waziri wa uchukuzi pamoja na mama Ida Odinga walikuwemo baadhi ya viongozi na ambao walizindua usafiri wa kampuni hii.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved