logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtumba Man asilimulia kwa uchungu jinsi mpenzi wake amekuwa akimdunda kama ngoma

ndoa ya vita yamlazimissha mitumba man kutorokea usalama

image
na

Habari25 September 2023 - 08:23

Muhtasari


• Katika mahojiano haya Mtumba man amesimulia kupitia mengi ikiwemo kuvunjwa kwa simu zake kwa madai ya hasira ya mpenzi wake.

Mtumba Man.
Mtumba Man.
Mtumba Man.

Baada ya Wakenya kutaka kujua tetesi za mtumba man  baada ya kuripoti kwa polisi huhusu kupigwa na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 22 na ambaye amemtaja kuwa wa mwaka wa nne katika chuo kikuu, stesheni ya Radio Jambo iliweza kumfikia.

Redio Jambo kupitia kipindi  cha Massawe Japanni  Mtumba man amekiri jinsi ambavyo mpenzi wake amekuwa akimpiga.

Kulingana naye wanaume wengi hupigwa jambo ambayo wengi uficha, lakini kwake limekuwa jambo ambalo limemkera sana.

Mtumba man amesimulia kuwa mpenzi wake amekuwa na mazoea ya kumpiga wakati ambao wanakuwa na ugomvi kidogo wa kifamilia ndani ya miaka miwili na ambayo wamekuwa kwenye mahusiano.

"Tumekuwa tukikorofishana kila wakati sababu kuu ni kuwa mpenzi wangu amekuwa tabia ya kuwa na mapenzi ya jinsia moja wakati mwigine uwaleta marafiki wake wasichana kwa nyumba yangu jambo ambalo ilinikera kwa muda mrefu." mtumba -man alisema.

Kulingana na jamaa huyu kichomfanya kuripoti jambo hili kwa polisi  ni wakati ambapo mpenzi wake alimpinga hadi mguu wake ukapatwa na majeraha wakati huu pia akisimulia  jinsi mwanamke huyu alimfuruta hadi kungoa baadhi ya nywele zake na kumugwara na kisu.

Katika mahojiano haya Mtumba man amesimulia kupitia mengi ikiwemo kuvunjwa kwa simu zake kwa madai ya hasira ya mpenzi wake.

"Kilichonitoa ni alama nyingi ndani ya mwili wangu ambazo nilipata kwa mahusiano haya kupigwa hadi kurushiwa visu na matusi kila siku," Mtumba man alisimulia.

Baada ya kuulizwa kama bado anampenda mpenzi aliweza kukiri kuwa kwa sasa mapenzi yamemchosha na angetaka awe na muda wake pekee ili kuweza kuwa na amani ndani ya maisha yake.

Mtumba Man.
Mtumba Man.
Mtumba Man.
Mtumba Man.

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved