Si mimi! Brian Chira akanusha madai video iliyochukiza

Chira amejitokeza kukana kabisa kuwa mtu kwenye video hiyo hakuwa yeye.

Muhtasari

•Mhusika katika video ambayo imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii aliwashangaza wengi alipoonekana kuvua nguo na kuanza kufanya mambo yasiyopendeza.

•Chira hakuamini jina lake lilikuwa likivuma kufuatia matukio anayoyafanya kwenye mitandao.

Brian Chira
Brian Chira

Brian Chira alivuma sana  wikendi iliyopita wakati video ya jamaa aliye uchi ambaye alidaiwa kuwa yeye ilisambaa kwenye mitandao.

Mwanatiktok huyo mwenye utata na amejitokeza kukana kabisa kuwa mtu kwenye video hiyo hakuwa yeye.

Wakati wa mahojiano na mwanablogu wa YouTube Ali, Chira hakuamini jina lake lilikuwa likivuma kufuatia matukio anayoyafanya kwenye mitandao.

Presenter Ali alimchezea kanda ya video hiyo inayoonyesha mambo machafu ambayo mhusika alifanya kwenye kipindi cha moja kwa moja katika juhudi za kupata ukweli.

Lakini hilo pia halikufua dafu, jambo ambalo lilimlazimu Ali kumtaka Chira kukiri waziwazi kuwa si yeye, jambo ambalo alilifanya bila hata aibu wala kutulia.

"Naapa yule sio mimi! Naapa yule sio mimi! Mimi! Ali!" Kisha akaendelea kumwambia Ali kwamba hakujua ni mtu yupi huyo aliyefanana sana na yeye.

Mhusika katika video ambayo imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii aliwashangaza wengi alipoonekana kuvua nguo na kuanza kufanya mambo yasiyopendeza kwenye kamera moja kwa moja.

Kitendo hicho kiliwakera wengi- huku baadhi wakitaka adhabu ya haraka kutoka kwa idara ya kuthibiti matumizi ya mitandao ya kijamii. 

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa X walidai kuwa Chira hakuwa sawa kisaokolojia na kwamba alihitaji sana msaada.