logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ex wa Flaqo afunguka kuhusu mchekeshaji huyo kuwa baba wa mtoto wake

Tracy alibainisha kuwa alipata mtoto wake baadaye baada ya kuachana na mchekeshaji Flaqo Raz.

image
na Radio Jambo

Habari03 October 2023 - 09:47

Muhtasari


•Tracy alisema Flaqo hakuwa na shida alipofahamu kuwa sasa yeye ni mama na kufichua kuwa alikuwa akimsaidia mtoto wake.

•Anne Tracy alibainisha kuwa alipata mtoto wake baadaye baada ya kuachana na mchekeshaji Flaqo Raz.

katika picha ya maktaba.

Mwanadada anayedai kuwa mpenzi wa zamani wa Flaqo Raz, Anne Tracy ameweka wazi kuwa mchekeshaji huyo si baba wa mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano.

Mama huyo wa mvulana mmoja aliwashirikisha wafuasi wake katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa Instagram siku ya Jumanne asubuhi ambapo alijibu maswali kadhaa kumhusu.

Mwanamitandao mmoja alitaka sana kujua kama Flaqo ni mzazi mwenzake, labda kwa sababu awali alisema kwamba alikuwa akimsaidia mtoto wake.

"Je, mfalme wetu mdogo ni wa Flaqo?" shabiki aliuliza.

Tracy akajibu kwa ujasiri, "Hapana."

Katika kipindi hicho, mrembo huyo pia alitangaza kuwa kwa sasa hayuko kwenye mahusiano na kuwaruhusu wanaume kujaribu kumtongoza ila kwa masharti fulani.

“Yes I am single. Please use your wallet to shoot those shots,” Tracy alimjibu shabiki aliyeuliza ikiwa anaweza kujaribu bahati yake naye.

Kumaanisha; “Ndiyo, niko single. Tafadhali tumia pochi yako kutupa mistari yako,”

Katika mahojiano ya hivi majuzi na Mungai Eve, Anne Tracy alibainisha kwamba alipata mtoto wake baadaye baada ya kuachana na mchekeshaji Flaqo Raz.

Mrembo huyo alisema Flaqo hakuwa na shida alipofahamu kuwa sasa yeye ni mama na kufichua kuwa alikuwa akimsaidia mtoto huyo licha ya kutokuwa baba mzazi.

“Mpoa wangu ako na miaka 5. Niko tu na huyo mpoa mmoja, my baby. Nilimpata baadaye, ako na miaka mitano hiyo nilimpata baadaye kabisa,” Tracy alisema.

Aliongeza, “Yeye (Flaqo) alikuwa sawa na hilo. Alikuwa anasupport at some point ata kama sio wake. Alikuwa akinisapoti wakati fulani. Alikuwa anatuma pesa ya birthday once in a while. Sio wake. Ni wangu pekee yangu.”

Tracy hata hivyo hakufichua baba mzazi wa mwanawe wala kuzungumzia zaidi kuhusu uhusiano wake wa sasa naye.

Akizungumzia uchumba wake na Flaqo, alisema kuwa walifahamiana kupitia mtandao wa Facebook mwaka wa 2016, wakachumbiana na hata kukaa pamoja kwa muda.

Alisema kuwa uhusiano wao uliisha baada ya yeye kurejea Nairobi kutoka Kisumu ambako alikuwa akiishi na mchekeshaji huyo.

“Tulikaa pamoja kwa muda. Tulifahamiana mwaka wa 2016. Sijui jinsi nilikwenda hadi Kisumu, lakini nilienda. Tulikuwa tunapendana, kwa hivyo nilihamia Kisumu Bondo. Alikuwa bado chuoni wakati huo," alisimulia.

Aliongeza, “Tuliishi kwa miezi michache lakini tulichumbiana kama mwaka mmoja. Kisha nikarudi Nairobi. I guess distance ikawa too much vitu zikaisha tu. Ilinibidi niende shule, ilinibidi niendelee na maisha yangu. Singekaa Kisumu niolewe ama nikae tu hivyo kama sifanyi chochote. Ilibidi nimerudi nisome.”

Anne Tracy alibainisha kuwa kuachana kwao yalikuwa ni makubaliano ya pande zote mbili bila vita na walibaki marafiki licha ya kwenda njia tofauti.

Alikiri kuwa anajuta kutokuwa mvumilivu na uhusiano wao na kutengana na msanii huyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved