Sina marafiki nimebaki tu na Mungu na "Wifi" - Brian Chira

Brian Chira amekuwa gumzo mitandaoni kwa video ambayo amekiri ilikuwa kwenye akaunti yake ya Instagram.

Muhtasari

• Chira kwa mara yingine kwenye mahojiana aliwaomba msamaha wafuasi wake na wanablogu wenzake waliomsaidia kujenga jina yake kwa mitandao ijapo aliwatukana.

Brian Chira
Brian Chira

Mwanatikoker Brian Chira kwa mara nyingine amejitokeza kwa mahojiano ya moja kwa moja kueleza jinsi maisha yake yamekuwa baada ya marafiki wengi kumuacha kwa kukerwa na vitendo vyake.

Mwanablogu wa mitandao Obina alieleza kuwa Brian Chira alimtafuta kwa blogu yake ili kumweleza changamoto anazokabiliana nazo.

"Marafiki wangu waliniacha naishi peke yangu nimebaki na mungu na simu mara mingi kwa nyumba yangu naomba tu mungu ,wakati usingizi unanilemea naingia kwa simu yangu,"alisema.

Chira kwa mara yingine kwenye mahojiana hayo aliwaomba msamaha wafuasi wake na wanablogu wenzake waliomsaidia kujenga jina lake kwa mitandao licha ya vitendo  vyake vya matusi.

"Naomba msamaha kwa wakubwa wangu nimekubali makosa yangu nataka tuishi vyema na marafiki wangu kwani  najiisi kuwa mpweke kila mara". Brian Chira alisema.

Kwenye mahojiano haya mwanaTiktoker huyo alisimulia kwamba ulevi umechangia machungu ambayo yamekera wanablogu wenzake ila aliwaomba akisema kuwa yuko tayari kubadilika .

Brian Chira amekuwa gumzo mitandaoni kwa video ambayo amekiri kuwa ilitumika katika akaunti yake, video hii ilionesha mtu kwenye akaunti ya Chira akitoa nguo na kushiriki tendo la kujichua.

Mwanatiktok Brian Chira
Image: RADIO JAMBO
Brian Chira
Brian Chira