Mganga asimulia jinsi anavyo tuma nyuki kunasa wezi

Nyuki Waswa kama alivyojitambulisha anasimulia kuwa na uwezo wa kutuma mtego wa nyuki.

Muhtasari

• Wakaazi mjini Kitengela walishagazwa na kisa  baada ya wanawake wawili   ambao waliripotiwa kuiba pesa  kutekwa na mtengo wa nyuki.

katika mji wa Kitengela mnamo Jumatano, Oktoba 4, 2023, Picha: KURGAT MARINDANY.
Washukiwa hao walifunikwa na kundi la nyuki katika mji wa Kitengela mnamo Jumatano, Oktoba 4, 2023, Picha: KURGAT MARINDANY.

Siku chache baada ya Mwanamke mmoja kupoteza Shilingi laki mbili na kuripoti kwa polisi na juhudi za kuwasaka wezi kukosa kufua dafu alitafuta huduma za mganga wa kienyeji.

 Mwanamke huyo aliyetabuliwa kwa jina Salome alisema alimpigia simu mganga mmoja ambaye wakati huo alikuwa Bungoma, na kumweleza hadithi yake.

 Mganga aliyetambuliwa kama  Nyuki Waswa alikubali kusafiri hadi Kitengela mnamo Oktoba 3, 2023, kumuhoji ili kujua kilichotokea.

Baada ya kumweleza kilichokuwa kimetendeka mganga huyu alimjulisha wezi hao walikuwa wanawake wawili na walikuwa wanasherekea kwa pesa hizo mjini Kitengela.

Kwa mshangao baada ya mganga huyo kufanya jaribio la kuwatuma nyuki alifahulu kuwasaka wezi hao.

Wakaazi mjini Kitengela walishagazwa na kisa hicho baada ya wanawake wawili ambao wanaripotiwa kuiba pesa hizo kutekwa na mtengo wa nyuki.

Mwanamke mmoja alikuwa na bunda la nyuki usoni huku wa pili akiwa na nyuki mkononi mwake.

 Nyuki Waswa kama alivyojitambulisha  alisema nyuki wake hawaumii wale anaowatumia bali huwachanganya wahalifu na wataendelea kuwa hivyo hadi atakapoitwa kuwaachilia huru “askari” nyuki wake.

Alisema wanawake hao wawili ambao walikamatwa na nyuki wake huko Kitengela walikuwa wakifurahia pesa hizo wakati askari nyuki walipofika kuwakamata.

Aisha Salome, mwanamke aliyepoteza Shilingi laki mbili katika basi lililokuwa likienda Kitengela kwa wezi wawili, alijawa na furaha kwa huduma za  mganga huyo.

 “Hakuna ninachofanya bali kuwaweka kwenye maombi. Nimeshindwa katika visa kesi nyingine kwa sababu washukiwa  wengi  husafiri mbali au hata nje ya nchi kupata huduma  za kinganga ili wanapo chukua mali ya watu wasije  wakajulikana "alisema.