Mhubiri wa kanisa la Life Church International Mchungaji T. Mwangi anapinga mila ya wanaume kulipa mahari kwa mwanamke anayenuia kuoa.
Baada ya wanablogu wa mitandao ya kijamii kutembelea mchugaji huyu kwa mahojiano ya moja kwa moja Kulingana na Mchungaji T wanaume wanafaa kujadiliana na wazazi wa wote ili kuafikiana lakini sio kulipa mahari.
"Dhana ya mahari ya kununua mwanamke ndio awe mke wako hufanya Mwanamke kukosa thamani kwa sababu mwanaume atakuwa na fikra baada ya kulipa mahali amemumiliki. Jambo hili litafanya mwanamke kukosa haki kwa familia, halifai kwa sababu wanawake watalinganishwa na chombo chochote cha kununua pale nyumbani, mbona wazazi wauze mtoto wao". alisema .
Mchungaji huyo alizidi kusema Wanaume hujiuliza maswali mengi wakati wa mkutano wa kulipia wanawake mahari kwa mfano wazazi wa mwanadada anayetaka kuolewa wanaweza kutaka Mbuzi au Ng'ombe kumi na kiasi cha pesa kama elfu kumi, jambo ili linaweza kuleta fikikra kwa akili ya mwanaume...kumfananisha mwanamke huyo kuwa wa thamani ya chini .
Alieleza kuwa ni aina ya utumwa, ambapo mwanamume hulipa pesa ili mwanamke awe mke wake.
Hapo awali Mchungaji T alisema hakumlipia mahari mkewe hata baada ya wakwe wachache kumlazimisha kufanya hivyo na hata kutuma wazee kuzungumza naye.