Mbunge Salasya aweka kikomo kejeli za `mwalimu wa Maths`

Salasya, alisisitiza kuwa walimu wamejitwika jukumu muhimu sana la kuunda mustakabali wa watu.

Muhtasari

• Salaysa alisema kejeli hizi zimevuma sana na zinachangia kudhalilisha heshima ya walimu hasa wa hisabti,ambao anadai wamechangia mafanikio ya watu wengi.

• "Walimu wamechukua jukumu kubwa katika maisha ya kila mtu,na ndio sababu wengi wao familia zao zimebarikiwa.Ndio maana pia wanahakikisha kwamba kila mmoja amefaulu maishani."

MBUNGE PETER SALASYA
Image: HISANI

Mbunge wa Mumias Mashariki,Peter Salasya ameeleza msimamo wake kuhusu mwenendo unaokua  wa Wakenya wanaotumia  msemo wa `mwalimu wa Maths` kuonyesha kwa mzaha mafanikio yao.

Salaysa alisema kejeli hizi zimevuma sana na zinachangia kudhalilisha heshima ya walimu hasa wa Hisabati,ambao anadai wamechangia mafanikio ya watu wengi.

Kweye video iliyoshirikishwa mitandaoni,alisisitiza kuwa walimu wamejitwika jukumu muhimu sana la kuunda mustakabali wa watu.

Salasya,alimshutumu Diana Marua kwa kutumia maneno haya ya kejeli kila mara wakati akionyesha mafanikio yake mitandaoni.

"Walimu wamechukua jukumu kubwa katika maisha ya kila mtu,na ndio sababu wengi wao familia zao zimebarikiwa.Ndio maana pia wanahakikisha kwamba kila mmoja amefaulu maishani."Alisema.

Aliongea kuwa walimu ndio msingi wa maisha bora hivyo wapewe heshima inayositahili.

"Tusiwatukane walimu wa Hisabati,kwa sababu huleta yaliyobora kutoka kwako,huyo ndiye msingi wako."

Alidokeza kuwa matani yanayoendelea kuhusu walimu wa Hisabati yanaweza kuleta aibu hasa wakiwa darasani na kuwataka watu kuonyesha heshima na shukrani kwao.

Msemo  huu ulipata umaarufu bada ya mwanamtandao mmoja kuanzisha maneno ya kumkosoa aliyekuwa mwalimu wake wa Hesabu,akisema mwalimu huyo alitabiri kuwa hawezi faulu maishani wakati akiwa shuleni.

Si muda mrefu  uliopoita ,Diana Marua,akaonyesha kutoridhika kwake na maisha yake ya zamani na kiwewe kilichosababishwa na mwalimu wake wa Hesabu.

Kwenye video iliyovuma mitandaoni,alionyesha kufadhaika kwake na kushiriki mafanikio yake ya mali licha ya matamshi ya aliyekuwa mwalimu wake wa Hesabu.

Mbunge Salasya amedai kwamba ni wakati mwafaka wakenya wakome kejeli hizo ili kukuza maudhui ya elimu mbayo ni muundo msingi wa watu katika jamii.