Mke mwenye hasira amwaga maji kitandani baada ya mumewe kukataa kumnunulia wigi (Video)

Mwanamke huyo alidai kwamba kwa kuwa marafiki zake walikuwa na wigi nyingi za kifahari, mume wake lazima pia amnunulie moja.

Muhtasari

• Tukio hili la kipekee halikuchukua muda kuenea katika majukwaa ya mitandao ya kijamii huku watumiaji wa mtandao wakishiriki mawazo yao.

• “Wanawake wengine wanakosa stara kabisa, ona sasa huyu anachagiza na akichapwa anasema ameonewa,” mmoja alisema.

Mwanamke amwaga maji kitandani.
Mwanamke amwaga maji kitandani.
Image: Screengrab

Mwanamke mmoja mwenye hasira amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kurekodiwa akivamia kitanda chake cha ndoa na mumewe na kukiloweza kwa maji.

Kwa mujibu wa video hiyo ambayo imevutia maoni kinzani katika mitandao ya kijamii, mwanamke huyo alipandwa na hasira baada ya ombi lake la kutaka kununuliwa wigi la kichwani na mumewe kukataliwa.

Kama njia ya kulipa kisasi, mke huyo alimwaga maji katika kitanda chote akimshinikiza mumewe kumnunulia wigi hilo kwa nguvu.

“Ni lazima utaninunulia wigi kwa nguvu,” kapsheni ya video hiyo ilisoma.

Video iliyokuwa ikisambaa mtandaoni, ikinasa mzozo mkali kati ya mwanamke huyo na mwanamume wake, ilizua hisia kubwa miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Mwanamke huyo alidai kwamba kwa kuwa marafiki zake walikuwa na wigi nyingi za kifahari, mume wake lazima pia amnunulie moja.

Tukio hili la kipekee halikuchukua muda kuenea katika majukwaa ya mitandao ya kijamii huku watumiaji wa mtandao wakishiriki mawazo yao.

“Wanawake wengine wanakosa stara kabisa, ona sasa huyu anachagiza na akichapwa anasema ameonewa,” mmoja alisema.

“Afanye hivi kwangu, siku hiyo anaenda kwa wazazi wake na ujeuri wote,” mwingine alisema.

“Jinsia pekee ambayo ilipinga kazi ya Mungu juu yao…… I heil oo” Olanyi Williams alisema.

“Anaweza kuwa anasumbuliwa na roho mbaya na anahitaji ukombozi wa jumla, ni kwamba sio wigi nzuri na nzuri kichwani mwake, naweza kufikiria ni wigi ngapi anavaa chumbani kwake hivi sasa, hata watoto wake wote wamemkatisha tamaa kitendo,” Defiat alisema.

Maoni yako ni yepi?