logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wakenya wamkejeli Diamond Platnumz kwa kukiharibu Kiingereza kwa mara nyingine

Wanawe Diamond walilia kwa uchungu alipowataarifu kuondoka.

image
na Samuel Maina

Burudani19 October 2023 - 12:21

Muhtasari


  • •Diamond alisikika akiwaeleza watoto hao wake wawili kwanini lazima wangeenda na mama yao nyumbani na hawangeweza kurudi naye nyumbani kwake.
  • •Diamond alijaribu kuwaeleza wanawe kuiwa ana shoo nyingine ya kufanya lakini Kiingereza alichotumia kujieleza kimewaacha wanamtandao wakimdhihaki.

Jumatano jioni, nyota wa bongofleva Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz alishiriki video yenye hisia kali akiwaaga watoto wake na mwanasosholaiti Zari Hassan, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Katika video hiyo, bosi huyo wa WCB alisikika akiwaeleza watoto hao wake wawili kwanini lazima wangeenda na mama yao nyumbani na hawangeweza kurudi naye nyumbani kwake.

Tiffah na Nillan ambao walionekana kuzidiwa sana na hisia walilia video nzima na kuweka wazi kuwa hawakutaka kutenganishwa na baba yao. Diamond hata hivyo aliwaambia kuwa ni lazima waende kuandaa mizigo yao na hati za kusafiria ili wawe tayari. kusafiri naye hadi Tanzania.

“Sitawaacha. Nikiondoka, mnichukie. Nikiondoka msizungumze nami. Naahidi sitaondoka nitakuwa hapa kesho. Itabidi muende na Mama T ili awapeleke katika ofisi ya uhamisho ili mpate hati za kusafiria,” alisikika Diamond akiwaambia watoto wake.

Tiffah hata hivyo hakuonekana kuridhika na kumtaka baba yake aeleze ni kwanini alitakiwa kuondoka na kutokuwa kwao.

Diamond alijaribu kuwaeleza kuwa bado ana shoo nyingine ya kufanya lakini Kiingereza alichotumia kujieleza kimewaacha wanamtandao wakimdhihaki.

Alisema, “I am going to do another sing.. and you in the morning you have to go with Mama T to get the passports. If you don’t get the passports you are not going to travel.”

Ni wazi kwamba Kiingereza cha mwimbaji huyo alipojieleza hakikuwa kizuri kwani alipaswa kusema "I am going to do another song/ I am going to sing again.”

Zari Hassan ambaye alikuwa amesimama hapo akiwa amewashika watoto wao alisikika akieleza kuwa staa huyo wa bongo fleva bado ana kazi ya kufanya.

Wanamtandao, hasa Wakenya wamekejeli Kiingereza duni cha mwimbaji huyo na jinsi anavyokiharibu kwa kujiamini.

Tazama maoni ya baadhi ya wanamitandao:

@djnassib Mna assume hiyo part ya “I am going to do another sing”

@lynetmusembi I am going to do another scene ama ni sin.

@obecheche_ninjaturtle He was doing well until that “another sing” ama maybe alikuwa ameshema “thing”

@idrin.ay Kilami nayo ameforce ya black Americans kabisa.

@munyokidoreen Nmekwama kwa another sing.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved