logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hakuna mwanamume anayechumbiana na mwanamke mmoja - Mwanamke mzee adai (video)

Alisema mapenzi ya kweli yaliisha mwaka 1980.

image
na Davis Ojiambo

Burudani26 October 2023 - 06:46

Muhtasari


  • β€’ Katika video, bibi anasisitiza kwa ujasiri kwamba ufahamu huu ni ishara ya ukomavu wa wanawake.
Mwanamke adai mapenzi ya kweli yaliisha 1980.

Mwanamke mmoja mkongwe mwenye lafushi ya Kinigeria amezua gumzo pevo katika mtandao wa X, awali ukiitwa Twitter baada ya video yake akitenganisha ukweli kutoka kwa uongo kuhusu suala la kuchumbiana na mapenzi kuenea.

Mkongwe huyo ambaye alikuwa anazungumza Kiingereza chenye lafudhi ya Pidgin alisema kwa ujasiri kwamba ameishi duniani kwa muda mrefu na wa kutosha kusema bayana kwamba hakuna mwanamume anayechumbiana na mwanamke mmoja, hata kama anaonekana zuzu asiyejitambua.

Bibi huyo alikwenda mbele pia kukiri kwamba hakuna mapenzi ya kweli katika kizazi cha sasa huku pia akifichua mwaka ambapo mapenzi ya kweli yalizikwa kwenye kaburi la sahau.

Katika video, bibi anasisitiza kwa ujasiri kwamba ufahamu huu ni ishara ya ukomavu wa wanawake.

Mwanamke huyo mzee, ambaye utambulisho wake haukufichuliwa, alisisitiza hoja yake kwa kusema kwamba hata kama mwanamume anaonekana kuwa hana hatia na mwenye mke mmoja, kuna uwezekano mkubwa anahusishwa na wanawake wengi kwa wakati mmoja.

“Ukomavu ni pale unapoelewa kuwa hakuna mwanaume anayechumbiana na mwanamke mmoja tu, hata aonekane hana hatia kiasi gani. Mapenzi ya kweli yaliisha mnamo 1980,” mwanamke mzee alisema kwenye video hiyo.

Video hiyo imezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku hisia tofauti zikimiminika kutoka kwa wanaume na wanawake.

Maoni ya Wanamtandao...

 

@youngskidmusic alisema; "Ahbeg ikiwa mwanamume anachumbiana na mwanamke mmoja, na mwanaume wa aina hiyo anasemekana kuwa na mke wa kiroho. Tafadhali je huyo mke wa kiroho ni mpenzi wake pia? πŸ˜‘πŸ˜‘β€

 

@el_daxxy alisema; "Upendo wa kweli haupatikani ... sasa ndoa ni mchezo wa viti vya enzi. Wakati wowote unapochoka. Unapakia comot."

 

@jaybaba009 alisema; "Mama huyu alikuwa olo namba 1 katika siku zake ... Mume wake anakwenda kumsikia ... Naam, anaweza kuwa anazungumza kutokana na uzoefu wake binafsi."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved