“Tukizaa alikuwa tu!” Karen Nyamu ataka mkewe Samidoh arudi 'waendelee mahali waliachia'

Seneta Nyamu alibainisha kuwa ikiwa mke wa Samidoh, wataendelea tu kutoka mahali walipoachia.

Muhtasari

•Mwanamitandao alimuonya seneta Nyamu huenda akaaibika sana wakati mpenzi Samidoh atampata mkewe tena.

•Seneta Nyamu alidokeza kuwa hata mwimbaji huyo wa Mugithi alipokuwa akimtunga mimba, mke wake alikuwa bado yupo.

 

Samidoh na Karen Nyamu
Image: HISANI

Jumatano jioni, seneta maarufu wa kuteuliwa Karen Nyamu alijibizana na wafuasi wake ambao walitoa maoni kwenye mojawapo ya machapisho yake kwenye mtandao wa Facebook.

Kuwaburudisha mashabiki wake, mwanasiasa huyo mwenye utata alichapisha posti la kuchekesha lililozungumzia jinsi mpenzi wake alidanganya kuhusu kwa nini anachukua muda mrefu kujibu jumbe zake za simu.

"Nimeuliza chali yangu mbona anachukua muda mrefu kujibu akaniambia yeye ni kigugumizi.. kimeanza kuniramba, na mlikuwa mumeniwoon," Karen Nyamu alichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumatano jioni.

Kama kawaida, mamia ya watumiaji wa mtandao walikusanyika chini ya chapisho lake na maoni tofauti, wengi wao wakitoa maoni kuhusu uhusiano wake wenye utata.

Mwanamtandao Evaline Wangari alimuonya kwamba huenda akaaibika sana wakati mpenzi wake Samuel Muchoki almaarufu Samidoh atampata mkewe tena.

"Subiri hadi apate yule halisi, utakuwa unatuona unabadilika mwelekeo #nothingbutprayers," mtumiaji huyo wa Facebook aliandika.

Katika majibu yake, seneta huyo wa kuteuliwa wa UDA alidokeza kuwa hata mwimbaji huyo wa Mugithi alipokuwa akimtunga mimba, mke wake alikuwa bado yupo.

Alibainisha kwamba ikiwa mke wa mwimbaji atarudi, wataendelea pamoja tu kutoka mahali walipoachia.

“Tukizaa alikuwa tu. Akuje tuendelee mahali tuliachia,” Karen Nyamu aliandika.

Mtumiaji mwingine wa Facebook, Irene Gatwiri, alitoa maoni, “Sio husband tena na uliachiwa?”

Akajibu, “Wacha kuniharakisha!”

Mwezi Julai, mke wa Samidoh, Edday Nderitu aliweka wazi kwamba alimuacha mumewe ili awe na mwanamke ambaye alionekana kumtaka zaidi.

"Wacha nifafanue mambo machache ambayo yalishirikiwa mtandaoni na sio sahihi. Siko kwenye ndoa ya wake wengi, kama ilivyoelezwa nilimuacha mume kwa yeyote aliyemhitaji zaidi,” Edday alisema kupitia Facebook.

Aliongeza, "Nilifanya uamuzi wa kujiondoa mimi na watoto wangu kutoka kwa mazingira hayo yenye sumu, haswa binti yangu kijana ambaye kwa bahati mbaya anapokea moja kwa moja tabia isiyoaminika iliyoonyeshwa."

Edday alisema hayo baada ya Nyamu kudai kuwa Samidoh na Edday Nderitu bado wako katika uhusiano mzuri na huwa wanazungumza.

Katika mahojiano na na Ala C kwenye kipindi cha Reke Ciume na Ene, seneta Nyamu alifichua kuwa Edday ambaye kwa sasa anafurahia wakati na familia yake nchini Marekani bado huwa anawasiliana na Samidoh na akadai kwamba hawezi kwenda popote kwani muungano wao hauwezi kuvunjika kwa urahisi.

“Mambo mnayoyaona kwenye mitandao ya kijamii mtashangaa sana, kuna baadhi ya miungano imetoka mbali sana. Labda hajui kwamba haendi popote, lakini najua kwa sababu miungano mingine si rahisi kukatika,” alisema.

Nyamu alidokeza kuwa mpenzi wake Samidoh na mkewe wa kwanza wamechukua mapumziko lakini bado wako katika uhusiano mzuri.

“Huwa naskia wakiongea, wako sawa sio vile mnafikiria. Hata watoto wanaongea naye kupitia simu yake. Kwa ground hakutawahi haribika,” alisema.

Seneta huyo alisisitiza kuwa yeye si mharibifu na akadokeza kuwa kuna mambo makubwa yatajidhihirisha katika siku zijazo.