Kisa cha aibu wakati makalio bandia ya mrembo yalianguka akiwa ananengua jukwaani (Video)

Ghafla densi ikiwa imeshika kasi makalio feki ya mrembo yule yaliporomoka na kutawanyika kwenye sakafu ya kucheza densi na kuwaacha wengi kwa vicheko.

Muhtasari

• Pindi alipoingia jukwaani na kuanza kucheza densi, mwanamume mmoja alimkaribia na kumuomba kucheza densi pamoja.

Makalio feki
Makalio feki
Image: Screengrab

Mwanamke mmoja mrembo alisalia na kovu la aibu la kudumu katika nafssi yake baada ya tukio la aibu kumfika akiwa katika kbalu cha starehe akipunja raha.

Kwa mujibu wa video ya tukio hilo ambayo imeenezwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii, mrembo huyo mwenye umri wa makamo alijitoma kwenye jukwaa wakati DJ aliweka muziki wake pendwa.

Alikuwa amevalia rinda la njano lililomchora vizuri maungo yake, lakini wengi hawakuwa wanajua kwamba makalio yale aliyokuwa nayo hayakuwa halisi bali ni ya kughushi tu.

Pindi alipoingia jukwaani na kuanza kucheza densi, mwanamume mmoja alimkaribia na kumuomba kucheza densi pamoja kufurahia muziki wa mapenzi.

Ghafla densi ikiwa imeshika kasi makalio feki ya mrembo yule yaliporomoka na kutawanyika kwenye sakafu ya kucheza densi na kuwaacha watu waliojaa katika klabu hicho kwa vicheko vya kustaajabu.

Video ya tukio hilo imezua vichekesho na maoni kinzani kutoka kwa watu huku wengi wakishauri kina dada kujisitiri kwa njia halisi ili kuepuka visa vya aibu kama hivyo.

Tazama video ya tukio hilo hapa chini.