Mrembo aonesha Range Rover mpya, akiri hakufanya bidii kuipata bali ni juhudi za 'mubaba'

Akionesha gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni 19 za Kenya, alisema kwamba yeye si yule mtu wa kudanganya kwamba 'Ooh Mungu mkubwa.. ooh bidii yangu' na kufichua kwamba ni kazi ya mubaba.

Muhtasari

• Gari lake jipya ni Range Rover Autobiography, ambalo ni modeli ya juu zaidi ya safu ya Range Rover.

• Gari inaendeshwa na injini ya lita 5.0 ya V8 ambayo inazalisha farasi 518 na torque 461 lb-ft.

Mrembo anunuliwa Range Rover na Mubaba
Mrembo anunuliwa Range Rover na Mubaba
Image: Instagram

Mwanasosholaiti mmoja amejitokeza katika mitandao ya kijamii na kusherehekea kupatiwa gari jipya aina ya Range Rover lenye thamani ya shilingi za Kenya milioni 19.

Cha kushagaza ni kwamba mrembo huyo alikiri wazi kwamba gari hilo wala hakutia bidii kaitka kazi yoyote ili kupatiwa bali ni juhudi za sugar daddy wake.

Tacha, Muigizaji wa Runinga kwenye kipindi kikubwa cha uhalisia maarufu kama BBNaija nchini Nigeria aliingia kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akifichua kuwa aliweza kupata dinga lake jipya, yote yakiwa ni kutoka kwa ‘Sugar Daddy’ wake.

Walakini, Tacha alijiunga na ligi ya watu mashuhuri wa Nigeria wanaomiliki magari ya kigeni huku akijigamba kuwa Range Rover yake ndiyo kubwa zaidi kuwahi kuonekana na ina thamani ya N100 milioni [shilingi milioni 19].

Gari lake jipya ni Range Rover Autobiography, ambalo ni modeli ya juu zaidi ya safu ya Range Rover. Gari inaendeshwa na injini ya lita 5.0 ya V8 ambayo inazalisha farasi 518 na torque 461 lb-ft.

Lina uwezo wa kubeba abiria watano na linakuja na vipengele mbalimbali vya kifahari, ikiwa ni pamoja na panoramic sunroof, viti vyenye joto na kupoa, na mfumo wa sauti wa Meridian.

Alishiriki picha yake akiwa na gari hilo jipya kwenye ukurasa wake wa Instagram, na nukuu, "New whip".

Pia alionyesha gari lake la Mercedes Benz kama alivyosema, "hatuuzi na kununua, tunanunua na kununua".

 

Tazama video hapa chini: