"Mume wangu ni Mnigeria!" Vera atangaza siku chache baada ya kuonekana na Burna Boy

Vera alikanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume yeyote Mkenya, akiwemo mzazi mwenzake Brown Mauzo.

Muhtasari

•Vera Sidika amekanusha madai kwamba bado anachumbiana na mzazi mwenzake, Fredrick Mutinda almaarufu Brown Mauzo.

•Vera alionekana kuwashambulia waeneza uvumi wanaomzungumzia na kuwataka waache kutumia jina lake kutafuta riziki.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika ameonekana kukanusha madai kwamba bado anachumbiana na mzazi mwenzake, Fredrick Mutinda almaarufu Brown Mauzo.

Katika taarifa fupi kwenye akaunti yake ya Instagram Jumatatu usiku, mama huyo wa watoto wawili alitangaza hadharani kwamba mpenzi wake ni Mnigeria.

Vera alionekana kukanusha tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume yeyote Mkenya, akiwemo mzazi mwenzake.

"Ninyi nyote lazima mmelewa na kitu fulani. Mume wangu ni Mnigeria, si Mkenya,” Vera alisema kupitia Instastori zake.

Wakati huohuo, alionekana kuwashambulia waeneza uvumi wanaomzungumzia na kuwataka waache kutumia jina lake kutafuta riziki.

"Watu wanahitaji KUACHA kuwa wafadhiliwa na watumiaji," alisema.

Aliongeza, "Kutumia jina langu kupanda na kutengeneza sarafu hakutasaidia."

Siku ya Jumanne wiki jana, Okt 31, Vera aliondoka kwenda Nigeria na alionyesha jinsi alivyotua katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Mwanasosholaiti huyo alionyesha kuwasili kwake Lagos, na ilisemekana kuwa alikuwa huko kwa sherehe. Sherehe hiyo ilijumuisha mwimbaji Burna Boy.

"Wakati wa kujitokeza," alinukuu video yake akiwa kwenye gari aina ya Lamborghini, ambayo inaaminika kuwa ya staa huyo wa Afrobeats.

Baadaye mama huyo wa watoto wawili alionekana katika kikundi cha watu wakiingia kwenye nyumba.

Katika video moja, Burna Boy alionekana akitembea kidogo mbele yake na inaripotiwa kwamba walikuwa pamoja.

Haya yanajiri zaidi ya miezi miwili baada ya habari za kutengena kwa mwanasosholaiti huyo na mzazi mwenzake, Brown Mauzo. 

Mwishoni mwa mwezi Agosti, Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Alishukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"