logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mummie Francie afunza Jinsi ya kushughulikia wanaume wa ku'cheat kwenye ndoa

Alishauri kwamba wakati umefika wa kugeuza hali ngumu ya mapenzi ambayo iko katika familia mbali mbali,

image
na Davis Ojiambo

Burudani07 November 2023 - 06:44

Muhtasari


  • • Aliwataka wanawake kutomwaga  machozi kamwe kwa kufadhaishwa na hali hiyo bali wajisatiti kupata ukweli.
  • • “Sasa tengeneza kundi la Whatsapp na umuongeze baba mkwe wako kama mtu wa kwanza kisha mama mkwe wako awe mtu wa pili,”
Muundaji wa Maudhui Mummie Francie

 Muundaji maudhui wa  TikTok  Mummie Francie amewashauri wanawake jinsi ya kukabiliana na wanaume wao wanaowalaghai na udanganyifu wa kimapenzi.

Katika video aliyopakia kwenye mtandao wa kijamii, mtayarishaji wa maudhui aliwataka wanawake kutomwaga  machozi kamwe kwa kufadhaishwa na hali hiyo bali wajizatiti kupata ukweli.

Alishauri kwamba wakati umefika wa kugeuza hali ngumu ambayo iko katika familia mbali mbali, na kuongeza kuwa wanawake wasio halalli katika maisha ya mwanamume, wamekuwa na ujasiri wa kuwaita wake wakuu na kuthibitisha msimamo wao.

“Sasa hatulii. Je, una data? kanunue  muda wa maongezi wa Sh20 pekee na uwe na Sh5 pekee kwenye M-pesa yako ya kutuma kwa side chick kuona jina lake kamili,” alianza.

Mummie alisisitiza kuwa  mchakato mzima utahitaji kuwa na maelezo kamili ya huyo mke ambaye wanafanya udanganyifu na mume wako na ikiwezekana picha zake.

“Sasa tengeneza kundi la Whatsapp na umuongeze baba mkwe wako kama mtu wa kwanza kisha mama mkwe wako awe mtu wa pili. Baada ya hayo ongeza wajomba wa mumeo, shangazi, binamu, kila mtu unayemfahamu ana uhusiano naye,” alisema.

Kisha akaongeza kuwa  huyo mke na mume wawe wa mwisho kuongezwa kwenye hicho kikundi ambacho alidai ni kamati ya kupanga sherehe za harusi.

“Baada ya kila mtu kuwa kwenye kikundi, ongeza mume wako na side chick yake. Hawa wawili wanapaswa kuwa wa mwisho kuongezwa. Sasa kila mtu akiongezwa, unaandika kwamba ‘hii ndiyo kamati itakayosimamia harusi ya fulani. Unajumuisha jina kamili la mumeo na la ukoo wake. Onyesha tarehe, mahali pa kanisa, saa, na hata mapokezi ambayo utakuwa umewapa.”

Mummie pia aliwaambia wanawake kwamba baada ya yote kusemwa na kufanyika, wanapaswa kuondoka kwenye kikundi cha WhatsApp na kusubiri shida kunyesha kama mvua ya radi.

Hii anasema ninjia moja ya kuwaadhibu watu wadanganyifu kwenye ndoa. "Mchungeni sana njia zenu maana tuna njama nyingi za kuwakomesha tabia hiyo," aliwaambia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved