"Shoe game ilikuwa juu!" Karen Nyamu afichua alivyokutana na Samidoh na kumpenda

Seneta Nyamu alimtaja mwimbaji huyo wa Mugithi kama mwanaume mwenye mahaba tele ambaye anamtendea kama malkia.

Muhtasari

• Karen alifichua kwamba mwimbaji huyo wa Mugithi alikuwa akitumbuiza katika hafla ambayo alikuwa amehudhuria wakati alipomtambua.

•Karen alisema alicheza mwanzoni alicheza na Samidoh mchezo wa kujificha na kutafuta huku akimpuuza na wakati huo huo kumpa vidokezo.

Samidoh na mpenziwe Karen Nyamu
Samidoh na mpenziwe Karen Nyamu
Image: HISANI

Seneta wa kuteuliwa Karen Njeri Nyamu amefichua kuwa alikutana kwa mara ya kwanza na mzazi mwenzake Samuel Muchoki almaarufu Samidoh katika hafla ya kisiasa iliyofanyika miaka kadhaa iliyopita.

Akizungumza kwenye YouTube Channel ya Convo, Karen alifichua kwamba mwimbaji huyo maarufu wa Mugithi alikuwa akitumbuiza katika hafla ambayo alikuwa amehudhuria wakati alipomtambua.

Seneta huyo alisema licha ya kumtambua mwanamuziki huyo, hata hivyo hawakupata fursa ya kuzungumza na kubadilishana namba mara ya kwanza walipokutana.

“Nilikuwa nimeona jina lake kwa YouTube lakini sikuwa shabiki hivyo ati namjua. Tulipatana tu kwa hafla fulani ya kisiasa ambapo alikuwa akitumbuiza, nikamtambua lakini hakuna chochote kilifanyika. Hatukubadilishana hata namba,” Karen Nyamu alisimulia.

Aliongeza, "Pia tulipata fursa nyingine, tukio lingine la kisiasa. Hiyo siku ndio niliona alaa, na kuna vile. Sijawahi kusahau hiyo shoe game kwanza. Ilikuwa juu. Mengine ni historia.”

Seneta huyo wa kuteuliwa wa chama cha UDA alisema wakati alipokutana na mpenzi wake huyo, alicheza naye mchezo wa kujificha na kutafuta kwa mara ya kwanza huku akimpuuza na wakati huo huo kumpa vidokezo.

Hata hivyo, hakufichua maelezo mengi ya nani alimwendea mwenzake kwanza.

“Iliflow tu!” alisema.

Katika mahojiano hayo hayo, Karen alimtaja mwimbaji huyo wa Mugithi kama mwanaume mwenye mahaba tele ambaye anamtendea kama malkia.

Mama huyo wa watoto watatu alifunguka kuhusu jinsi mpenziwe anavyomuonyesha mapenzi ikiwa ni pamoja na kumnunulia maua na kwenda naye kujiburudisha.

"Huwa ananunua maua, ananiambia anakuja kunichukua, tunaenda mahali kuna muziki tunakula, tunakunywa cocktails, tunacheka, sisi wawili tu alafu tunaenda nyumbani," Karen Nyamu alifichua.

Huku akizungumzia sifa anazopenda kwa mpenzi huyo wake, Seneta Nyamu alimsifu na kufichua kuwa ana vibe ya kuvutia sana ambayo anaipenda.

“Yupo poa, ana roho poa, anachekesha sana, ni muwazi, hajidai, roho iko uchi unaona. Ana vibe ambayo sijawahi kuona maishani mwangu. Anavutia sana. Kwa kawaida huwa anasema baadhi ya mambo na najua maishani mwangu sitawahi kusikia mtu mwingine akiyasema. Kwa kawaida mimi humwambia hivyo," Nyamu alisema.