Huddah Monroe awaonya wanadada dhidi ya kuzaa kabla ya kufikisha miaka 35, ataja sababu

Huddah amewataka wanawake wasikimbilie kupata watoto huku akiwaonya kuhusu wanaume wasiowajibika.

Muhtasari

•Mwanasosholaiti Huddah Monroe amewashauri wanadada kusubiri hadi watimize umri wa miaka 35 kabla ya kufikiria kupata mtoto.

•“Asilimia 90 ya wanawake ni wazazi single. Na si kwa hiari, wengine ni wazazi wasio na waume ndani ya ndoa,” Huddah alisema.

Image: INSTAGRAM// HUDDAH MONROE

Mwanasosholaiti maarufu wa Kenya Huddah Monroe amewashauri wanadada kusubiri hadi watimize umri wa miaka 35 kabla ya kufikiria kupata mtoto.

Katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 31 aliwashauri wasichana kutumia mbinu za kuzuia mimba wakati wakijihusisha na mapenzi hadi wafikie umri aliopendekeza.

Huddah ambaye anaendesha duka la bidhaa za urembo amewataka wanawake wasikimbilie kupata watoto huku akiwaonya kuhusu wanaume wasiowajibika.

"Wanadada wadogo, tafadhali msiwe na mtoto kabla ya umri wa miaka 35. Nenda upange uzazi, piga simu kwa mtaalamu wa njia ya uzazi hata. Atashauri,” Huddah alisema kupitia akaunti yake ya Instagram.

Aliongeza, "Usikimbilie na kuleta mtoto katika ulimwengu huu wa fujo. Watu wanatakiwa wajitafute wenyewe na Mungu kabla hawajapata dada yako tumboni."

Mwanasholaiti huyo mrembo ambaye kwa sasa anaishi Dubai alibainisha kuwa ni wanawake wengi ambao wanalea watoto peke yao bila uwepo wa wazazi wenzao.

“Asilimia 90 ya wanawake ni wazazi single. Na si kwa hiari, wengine ni wazazi wasio na waume ndani ya ndoa,” alisema.

Kufuatia hayo, Huddah aliwaomba wanawake wajiepushe na kupachikwa mimba akisema,, "Tazama mtindo huu na ufunge miguu yako hadi ujue unaweza kushughulikia mambo yako."

Mlimbwende huyo pia alionya kuwa kuzaliwa kwa watoto husababisha matatizo ya kisaikolojia kwa wazazi, hasa wanawake.

Huddah ambaye sasa ana umri wa miaka 31 bado hana mtoto. Uhusiano wake pia umebaki kuwa kitendawili ambacho hakijatatuliwa.

Mapema mwaka huu, mwanasosholaiti huyo anayeishi Dubai alibainisha kuwa ndoa si ndoto yake akiashiria kuwa si jambo rahisi.

Wakati huohuo, Huddah alifichua kwamba hata ikiwa angechukua hatua ya kuingia kwenye ndoa, angeiweka faragha mbali na macho ya umma.

“Umeshawahi kujiuliza si ndoto ya kila mtu. Ndoa sio matembezi kwenye bustani (si rahisi). Ni ngumu kuliko unavyofikiria. Na kama ningeolewa usingejua. Hilo litakuwa la faragha milele,” Huddah Monroe alisema.

Mfanyibiashara huyo mahiri wa bidhaa za urembo kwa muda mrefu amekuwa msiri sana kuhusu mahusiano yake.