Mhubiri wa kanisa la Life Church International, Mchungaji T Mwangi amesimulia jinsi Mungu alimuepesha na virusi vya ukimwi licha ya kushiriki mapenzi na wanawake wawili tofauti waliokuwa na virusi hivyo.
Mchungaji huyo alisimulia hayo huku akisema kuwa matukio hayo yalitokea kabla ya kuokoka na kuyaacha mambo ya dunia.
Anakumbuka Krismasi moja ambapo aliondoka nyumbani kuelekea klabu.
"Nilienda klabu na kitu cha kwanza kutokea ni kupigana, chupa ya pombe ikarushwa, kwa bahati nzuri niliponea."
Kiongozi huyo wa kanisa alisimulia jinsi alivyokutana na mwanamke ambaye alifanya naye mapenzi na baadaye akafariki kutokana na virusi vya ukimwi.
Ulikuwa ni msimu wa Krismasi, nilikuwa nimelewa na nikalala na mwanamke ambaye sikujua alikuwa na virusi vya ukimwi, baadaye tulimzika mwanamke huyo.
Mchungaji huyo alisimulia kuingia kwenye uhusiano mwingine na mwanamke ambaye alikuwa ameambukizwa virusi na Sugar Daddy.
"Nilianza kuchumbiana na mwanamke mwingine na jambo lile lile tena likajitokeza ,Niliambiwa kuwa mwanamke alikuwa ameambukizwa virusi na "sugar daddy "na alikuwa mgonjwa,"alisema.
Pasta huyo alisema kuwa cha kushangaza ni kuwa wakati alipoenda kufanya vipimo vya ugojwa wa ukimwi alipatikana kuwa hasi kwa neema ya Mungu.
"Nilienda "VCT" kupimwa cha kushangaza nikawa bila virusi kwa Neema ya Mungu,Jinsi Bwana alivyonihifadhi, sijui,"alisema.