Akothee athibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na Nelly Oaks baada ya ndoa na Omosh kufeli

Akothee alijigamba kuhusu mapenzi ya Nelly Oaks kwake na pia kukejeli ndoa yake iliyovunjika na Denis ‘Omosh’ Schweizer.

Muhtasari

•“Hapatikani, amechukuliwa! Kwa nini mnang’ang’ania Nelly Oaks. Si muende mchukue Omosh," Akothee aliwaambia wanaommezea mate Nelly Oaks.

“Kweli nikupatie namba ya Nelly? unadhani mimi nimetosheka? Mimi sijarudi soko, mimi ndiye soko, sigawani na mtu,” Akothee alisema.

na meneja wake Nelly Oaks.
Akothee na meneja wake Nelly Oaks.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki Esther Akoth almaarufu Akothee ameonekana kuthibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na meneja wake wa muda mrefu Nelly Oaks katika kipindi cha moja kwa moja cha hivi majuzi kwenye mtandao wa TikTok.

Katika kipindi hicho ambacho alikuwa akiwahutubia mashabiki wake Nelly Oaks akimwandalia chakula maalum jikoni, Akothee alisikika akimwita meneja huyo wake ‘babe’ mara kadhaa, jina ambalo hutumika sana sana  wapenzi.

Nelly Oaks pia alisikika akimtaja Akothee kama mtu maalum kwake huku wawili hao wakishiriki matukio ya kimapenzi kwenye kamera.

“Hiki ni chakula cha jioni maalum kwa mtu maalum kama wewe. Ni surprise,” Nelly Oaks alisikika akimwambia mwanamuziki huyo.

Wakati wa kipindi hicho, Akothee kwa hasira aliwasuta wanawake wote waliokiri mapenzi yao kwa meneja huyo wake akidokeza kuwa hapatikani kwao.

Wakati baadhi ya mashabiki walipotaka kujua iwapo Nelly Oaks ana mchumba, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alionekana kuthibitisha kuwa yeye ndiye anashikilia nafasi hiyo.

“Ati kama Nelly ako na mtu?! Kwani mimi mawe? Mimi mawe? Ama mimi ni mti? Unauliza kama Nelly ako na mtu, kwani mimi ni mawe? Ama kijiti? Usinipimie pumzi. Maisha ni ya kwangu nayaendesha vile nataka,” alisema.

Mama huyo wa watoto watano pia alikataa ombi la nambari ya simu ya Nelly Oaks huku akifichua kwamba hata ana uwezo wa kufungua na kutumia simu yake.

“Kweli nikupatie namba ya Nelly? unadhani mimi nimetosheka? Mimi sijarudi soko, mimi ndiye soko, sigawani na mtu,” Akothee alisema.

Nelly Oaks pia aliweka wazi kuwa hapatikani kwa mwanamke mwingine.

Akothee aliwaambia kwa kejeli wanamke waliomtaka meneja wake badala yake wamtafute aliyekuwa mumewe, Denis Schweizer ambaye alibainisha kuwa hana mchumba kwa sasa.

“Hapatikani, amechukuliwa! Kwa nini mnang’ang’ania Nelly Oaks. Si muende mchukue Omosh, muende mchukue Omosh wa Pakistan. Yeye ndiye ako single,” alisema.

Aidha, mwanamuziki huyo alisikika akijigamba kuhusu mapenzi ya Nelly Oaks kwake na pia kukejeli ndoa yake iliyovunjika na Denis ‘Omosh’ Schweizer.

“Ni vizuri sana kupendwa, nilikuwa nimeenda huko (to Schweizer) nikifikiria ni , ati greener pastures, kimenichoma!!.. Ati mzungu wueh! Kumbe mzungu!,” Akothee alisema.

Aliendelea kuzungumzia masaibu yake na aliyekuwa mume wake mzungu akisema, “Mzungu karibu anitoe roho, nitakuja kuwaelezea siku moja.”