Jamaa awashangaza wengi kwa ustadi wa ku'balance hotpots zaidi ya 20 kichwani akitembea

Hotpots hizo zilikuwa zimepangwa kwa namna ambayo kila moja ilikuwa imeingizwa ndani ya nyingine lakini pia kuna zingine ambazo zilikuwa zimening’inizwa kando

Muhtasari

• “Mwanaume huyo alipanga hotpots 20 zaa ukubwa tofauti na kubeba kichwani kwa namna iliyohitaji ustadi,” video hiyo ilisema.

Jamaa muuza hotpots
Jamaa muuza hotpots
Image: TikTok

Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo amewashangaza wengi baada ya video yake kuibuka akiwa amebeba hotpots kubwa Zaidi ya ishiriki kichwani tena kwa ustadi mkubwa barabarani.

Video hiyo iliyopakiwa kwenye mtandao wa TikTok na mtumizi kwa jina Dynamic Eagle ilionesha kijana huyo akikatiza barabarani katika kile kilitajwa kama alikuwa anaelekea sokoni kuuza shehena hiyo ya hotpots.

Kilichowashangaza wengi ni kwa jinsi aliweza kuzipanga hotpots hizo na kuwa kama mlima mrefu kichwani na umahiri ambao alitumia kuzibeba zote kwa pamoja pasi na moja yao kudondoka.

“Mwanaume huyo alipanga hotpots 20 zaa ukubwa tofauti na kubeba kichwani kwa namna iliyohitaji ustadi,” video hiyo ilisema.

Hotpots hizo zilikuwa zimepangwa kwa namna ambayo kila moja ilikuwa imeingizwa ndani ya nyingine lakini pia kuna zingine ambazo zilikuwa zimening’inizwa kando katika pande zote mbili katika picha ambayo kwa haraka mtu atadhani zilikuwa zimefungwa ili kuzizuia zisidondoke.

Msimulizi katika video hiyo alimsifu kijana huyo kwa ubunifu wake wa kusisimua. Msimulizi pia alisema alichokifanya si uchawi bali ni sehemu ya ustadi wake wa kuhangaika mitaani kutafuta riziki.

Tazama video hii hapa chini msimulizi akisisitiza kwamba huo si ushirikina