Ni ushamba? Mrembo ashindwa kutumia lift hadi kumlazimu soja kumsaidia kupanda (video)

Kwa muonekano wa mambo, mrembo huyo alikuwa hajawahi tumia ngazi za aina hiyo zinazowezeshwa na mfumo wa umeme, au ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuja ana kwa ana na teknolojia ya aina ile.

Muhtasari

• Mrembo huyo alikuwa anatoka orofa ya chini akielekea katika orofa za safu ya juu na alilazimika kutumia lift ya aina ya ngazi za kukwea.

Ngazi za stima,maarufu lift
Ngazi za stima,maarufu lift
Image: TikTOK

Mijengo ya siku hizi na haswa ile ambayo ni ya kibiashara katika mitaa ya kifahari ina mitambo ya kufanya urahisi kwa watu na mizigo kukwea kutoka orofa moja kuelekea nyingine, kwa kimombo lift.

Zipo lift za kawaida ambazo mtu anaingia ndani na kupandishwa lakini kuna zingine ambazo zimeundwa kwa mfano wa ngazi za kupandia ambapo mtu anasimama kwenye ngazi ya chini ya kupandishwa katka hali ya mzunguko.

Sasa kuna video moja ambayo imezua vichekesho katika mtandao wa TikTok ikimuonesha mrembo mmoja aliyekuwa amevalia nadhifu na kwa dalili zote kuonekana mtu mwenye akili zake timamu na uelewa wa mambo.

Mrembo huyo alikuwa anatoka orofa ya chini akielekea katika orofa za safu ya juu na alilazimika kutumia lift ya aina ya ngazi za kukwea.

Katika hali ya kustaajabisha, mrembo yule alifika kwenye eneo la lift na alichoona ni ngazi zile zikipanda na upande mwingine zingine zilikuwa zinateremka kwa usanjari.

Alionekana kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja akijaribu kutia wayo wake kwenye ngazi moja na kuona inavutwa na ngazi kwenda juu kabla ya kuondoa mguu wake kwa ghafla na haraka.

Kwa muonekano wa mambo, mrembo huyo alikuwa hajawahi tumia ngazi za aina hiyo zinazowezeshwa na mfumo wa umeme, au ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuja ana kwa ana na teknolojia ya aina ile.

Ilimbidi mlinzi wa karibu kufika kumpa msaada.

Mlizni yule alifika na kumshika mkono kwa hali ya kumpa hakikisho kwamba asingedhurika kwa njia yoyote ile kabla ya kuingia na yeye kwenye ngazi na kumuonesha jinsi ya kushikilia ili kupelekwa katika safu ya juu ya orofa.

Video hiyo imevutia maoni mbali mbali ya vichekesho na wengine hata hivyo wakisema kwamba mrembo huyo huenda alimpa mtu simu kumrekodi ili kujifanya kuwa hajawahi kutana na ngazi za aina ile.