logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Binti yangu angekuwa rehab, ningekuwa nimezikwa" Edday amshukuru Bernice Saroni kwa kumsaidia kuhamia Marekani

Bernice pia aliweka wazi kuwa anajivunia kumsaidia Edday kuhamia Marekani.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri25 November 2023 - 11:06

Muhtasari


•Huku akimshukuru Saroni kwa ukarimu wake, mama huyo wa watoto watatu alisema kwamba alichomfanyia hakiwezi kuelezewa kwa maneno tu.

•Mburudishaji huyo anayejitambulisha kama ‘Mamake Boyz’ aliweka wazi kuwa anajivunia kumsaidia Edday kuhamia Marekani.

Mke wa kwanza wa mwimbaji maarufu wa Mugithi, Samidoh, Edday Nderitu amemshukuru Bernice Saroni kwa kumsaidia kuhamia Marekani mapema mwaka huu.

Huku akimshukuru Saroni kwa ukarimu wake, mama huyo wa watoto watatu alisema kwamba alichomfanyia hakiwezi kuelezewa kwa maneno tu.

Edday alidai kwamba ikiwa mhudumu huyo wa afya hangemsaidia, labda kufikia sasa angekuwa amekufa na binti yake angekuwa katika hali mbaya.

“Mungu akubariki Bernice, chochote ulichonifanyia mimi na watoto wangu ni kitu ambacho siwezi kukieleza. Binti yangu angekua rehab na mimi ningekuwa futi 6 chini,” Edday Nderitu alisema kupitia mtandao wa Tiktok.

Mama huyo wa watoto watatu ambaye amekuwa Marekani kwa miezi kadhaa iliyopita alikuwa akimtetea Bernice kwa madai kwamba alisaidia kuvunja ndoa yake.

Siku ya Ijumaa, Bi Saroni alijibu madai ya kumtoa Edday Nderitu katika ndoa yake ya miaka mingi na Samidoh kwa sababu yeye pia ni mama asiye na mwenzi.

Katika video ambayo alishiriki kwenye TikTok, mburudishaji huyo anayejitambulisha kama ‘Mamake Boyz’ aliweka wazi kuwa anajivunia kumsaidia Edday kuhamia Marekani.

"Sidechick. Si hii kitu imewauma. Na hamtoshekangi. Kwa kweli ninajivunia sana kwa kile nilichomfanyia. Kumleta Marekani, unafikiria kukuja Marekani ni rahisi, na kuja mpaka na watoi. Ninajivunia sana. Ngoja nikwambie kitu kimoja, leo ikiwa siku ya kutoa shukrani, jambo moja ambalo namshukuru Mungu ni kwa Edday kuwa Marekani,” Bernice alimjibu mtumiaji wa Tiktok ambaye alimshutumu kwa kumfanya Edday atoke kwenye ndoa yake.

Aliongeza “Huoni vile siku hizi anang’aa, huoni vile watoto wake wanang’aa. Ama hata hujamuona hivi majuzi, ebu enda kwa page yake uone vile anakaa vizuri. Anakaa tu doh, amebarikiwa, ana furaha na ana amani. Alafu unafikiria nitahisi vibaya, ati juu mimi ni single mum mnanihukumu ati nilimtoa kwa boma lake. Hebu niambie wewe unafanyia nini familia yako. Unasaidia familia yako au unawaua kwa maneno yako. Kweli wewe unakaa wale watu wa kusengenya tu familia yako. Hebu niambie, sisi tunaeneza upendo. sawa.”


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved