logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Career mpya huanza hivi" Karen Nyamu ajawa bashasha huku akishirikishwa kama vixen kwenye wimbo (+video)

“Niko kwa wimbo wa subukia, career mpya huanza hivi sasa. Good one Sarafina Salim, I am so emotional,” Karen Nyamu alisema.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri25 November 2023 - 08:48

Muhtasari


•Karen Nyamu alishirikishwa kama vixen na msanii maarufu wa nyimbo za Kikuyu, Sarafina Salim katika mojawapo ya nyimbo zake.

•“Niko kwa wimbo wa subukia, career mpya huanza hivi sasa. Good one Sarafina Salim, I am so emotional,” Karen Nyamu alisema.

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu hivi majuzi alishirikishwa kama video vixen na msanii maarufu wa nyimbo za Kikuyu, Sarafina Salim katika mojawapo ya nyimbo zake.

Katika wimbo wake ‘Ruo rwa muciari’ (Uchungu wa mzazi), alioutoa takriban wiki moja iliyopita, mwanamuziki Sarafina Salim alimtaja mwanasiasa huyo mtata na kumuonyesha kwa muda mfupi kwenye video ya muziki huo.

Mwimbaji huyo wa muziki wa Kikuyu katika wimbo huo alimuomba seneta Karen Nyamu kuendelea kuwalea watoto wao vizuri.

“Seneta Karen Nyamu, uturerere twana twitu nginya twigane,” Sarafina Salim aliimba.

Kumaanisha: "Seneta Karen Nyamu, tulelee watoto wetu hadi wakue."

Wakati akisherehekea kushirikishwa kwenye wimbo huo, seneta huyo wa UDA alidokeza kuwa kazi mpya ya video vixen huenda ikaanza hivyo tu kimzahamzaha.

“Niko kwa wimbo wa subukia, career mpya huanza hivi sasa. Good one Sarafina Salim, I am so emotional,” Karen Nyamu aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuwaelekeza wafuasi wake wapi wangetazama wimbo huo kwenye YouTube.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya mama huyo wa watoto watatu kudokeza kuwa huenda hatawahi kuonekana kwenye video za muziki za mzazi mwenzake, Samuel Muchoki almaarufu Samidoh ambaye pia ni mwimbaji wa muziki wa Kikuyu anayebobea na aina ya muziki ya Mugithi.

Wakati akiongea katika mahojiano ya hivi majuzi, mama huyo wa watoto watatu alibainisha kuwa yeye na mwimbaji huyo wa Mugithi huwa hawachanganyi mahusiano yao na kazi.

"Hizo ni kazi. Hatuchanganyi kazi na mapenzi,” Karen Nyamu alisema wakati wa mahojiano kwenye YouTube channel ya Convo.

Aliongeza, "Hiyo ni kazi, iko serious!"

Katika mahojiano hayo, Karen Nyamu ambaye hajaona aibu kuweka mahusiano yao wazi alikiri kuwa hata baada ya mahusiano yake na baba huyo wa watoto wake wawili kujulikana hadharani miaka michache iliyopita, alijaribu sana kumtema mwimbaji huyo lakini kila mara moyo wake bado ungemrudisha kwake.

"Ogopa roho! Humjui vizuri!" alisema.

Alisema kuwa uhusiano wao ni muunganisho wa asili tu na akaweka wazi kwamba anafurahi juu yake. Pia alibainisha kuwa hayuko kwenye uhusiano kwa sababu ya pesa kwani wote si masikini.

Akizungumzia sifa anazopenda kwa mpenzi huyo wake, Seneta Nyamu alimsifu na kufichua kuwa ana vibe ya kuvutia sana ambayo anaipenda.

“Yupo poa, ana roho poa, anachekesha sana, ni muwazi, hajidai, roho iko uchi unaona. Ana vibe ambayo sijawahi kuona maishani mwangu. Anavutia sana. Kwa kawaida huwa anasema baadhi ya mambo na najua maishani mwangu sitawahi kusikia mtu mwingine akiyasema. Kwa kawaida mimi humwambia hivyo," Nyamu alisema.

Karen alifichua kwamba alikutana na Samidoh kwa mara ya kwanza katika hafla ambapo alikuwa akitumbuiza kabla ya kufahamiana vyema baadaye.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved