logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Ni mwongo!" Edday Nderitu amwaga mtama kuhusu Karen Nyamu kumsaidia kupata zabuni za serikali

Karen Nyamu alidai alishirikiana na kakake Samidoh kusaidia katika mchakato wa kuwasilisha stakabadhi na kupata zabuni.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri26 November 2023 - 07:51

Muhtasari


•Edday Nderitu amekanusha vikali kusaidiwa na seneta Karen Nyamu kupata zabuni ya serikali ya Ksh9milioni.

•Karen Nyamu alidai alishirikiana na kakake Samidoh kusaidia katika mchakato wa kuwasilisha stakabadhi na kupata zabuni.

Mke wa kwanza wa mwimbaji Samidoh, Edday Nderitu amekanusha vikali kusaidiwa na seneta Karen Nyamu kupata zabuni ya serikali ya Ksh9milioni.

Katika mahojiano na Bonga na Jalas mnamo 2021, seneta huyo wa kuteuliwa ambaye sasa ana watoto wawili na aliyekuwa mume wa Bi Edday Nderitu kwa takriban miaka 15 alidai kwamba alimsaidia mama huyo wa watoto watatu kupata zabuni ya serikali ya kusambaza vifaa vya maandishi vya thamani ya mamilioni ya pesa.

Seneta Nyamu alidai kwamba alishirikiana na kakake Samidoh kusaidia katika mchakato wa kuwasilisha stakabadhi na kupata zabuni.

“Ninawezaje kumchukia mtu ambaye nilimsaidia? Mwaka jana (2020), nilimpa Samidoh wazo kwamba yeye (Edday Nderitu) asajili kampuni kwa sababu tulikuwa tukipata zabuni. Hivi sasa anatoa zabuni ya vifaa vya kuandikia vya thamani ya Sh9 milioni ambayo mimi na kakake Samidoh Kariz Magic tuliketi na kutengeneza stakabadhi hizo,” Karen Nyamu alidai wakati wa mahojiano na Jalang’o.

Wakati wa mahojiano hayo yaliyofanyika miaka miwili iliyopita, alikana pia kuwa mvunja ndoa na kusisitiza kwamba kila mara alikuwa akimsapoti Edday.

Katika sehemu ya maoni ya video iliyochapishwa hivi majuzi na Bernice Saroni kwenye Tiktok, shabiki mmoja aliibua madai ya hapo awali ya seneta Nyamu kuhusu kumsaidia mke wa muda mrefu wa Samidoh kupata zabuni za serikali.

“Kuna wakati Nyamu alisema kuwa Edday anapata zabuni kupitia kwake, labda ndiyo maana Edday hakuweza kuondoka. Lakini kwa nini Edday aliishia USA ni Mungu anajua zaidi,” shabiki aliandika.

Wakati akijibu maoni hayo, Edday Nderitu alidai kuwa seneta huyo wa kuteuliwa wa UDA ni muongo sana.

"Je, nilionekana kama milioni 9 nikiwa Kenya? Asilimia 99 ya anachozungumza ni uongo, ulizia kwa ground rafiki yangu,” Edday alisema.

Katika chapisho hilo, dday Nderitu alimshukuru rafiki yake Bernice Saroni kwa kumsaidia kuhamia Marekani mapema mwaka huu.

Huku akimshukuru Saroni kwa ukarimu wake, mama huyo wa watoto watatu alisema kwamba alichomfanyia hakiwezi kuelezewa kwa maneno tu.

Edday alidai kwamba ikiwa mhudumu huyo wa afya hangemsaidia, labda kufikia sasa angekuwa amekufa na binti yake angekuwa katika hali mbaya.

“Mungu akubariki Bernice, chochote ulichonifanyia mimi na watoto wangu ni kitu ambacho siwezi kukieleza. Binti yangu angekua rehab na mimi ningekuwa futi 6 chini,” Edday Nderitu alisema kupitia mtandao wa Tiktok.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved