Mshangao huku dadake Akothee, Cebbie Koks akiweka chuki kando na kumsherehekea

Cebbie alimtambua Akothee hadharani kama dadake kipenzi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.

Muhtasari

•Cebbie Koks alisherehekea safari ya elimu ya Akothee na kueleza fahari yake kwa mafanikio makubwa aliyoyapata.

•Licha ya kuwa ndugu, Cebbie Koks na Akothee hawajawa katika uhusiano mzuri katika miaka michache iliyopita.

alihitimu Ijumaa.
Akothee alihitimu Ijumaa.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Dada mdogo wa Akothee, Cebbie Koks Nyasego aliwashangaza Wakenya wengi siku ya Ijumaa baada ya kuweka chapisho refu kwenye mtandao wa Instagram akimpongeza mwimbaji huyo kwa kuhitimu kutoka Chuo Kikuu.

Akothee alitawazwa na shahada katika usimamizi wa biashara katika Chuo Kikuu cha Mt Kenya Ijumaa baada ya kusoma katika shule hiyo ya kibinafsi kwa miaka kumi na minne.

Huku akimpongeza dada yake mkubwa kufuatia fanikio hilo, Cebbie Koks ambaye kwa muda mrefu imekuwa ikisemekana kuwa haelewani na mwanamuziki huyo alisherehekea safari yake ya ajabu na ngumu ya elimu na kueleza fahari yake kwa mafanikio makubwa aliyoyapata.

"Leo ni hatua muhimu katika safari yako ya kielimu unapohitimu na digrii ya bachelor. Ninajivunia sana na kujitolea ulikoonyesha. Elimu kweli ni nguvu yenye nguvu na umekubali kikamilifu uwezo wake. Umeamini daima katika nguvu ya mabadiliko ya ukuaji wa kibinafsi. Nakumbuka "Toto 649," aah! Hiyo ndiyo maana ya leo 😂😂😂na unajua jinsi ilivyokuwa ya kufurahisha,” Cebbie Koks aliandika.

Aliongeza, “Nimekuwa na bahati ya kushuhudia ukuaji na maendeleo yako moja kwa moja. Nimekuona ukikabiliana na changamoto nyingi kwa dhamira, uvumilivu, na roho isiyoyumba. Uwezo wako wa kurudi nyuma kutoka kwa shida umekuwa wa kushangaza sana.

Leo, unapovaa kofia na gauni maridadi, nataka ujue kuwa mafanikio haya ni miongoni mwa urithi wako mkubwa. Ninajua pia kwamba umetimiza mambo ya ajabu, na jina lako limetambuliwa katika machapisho mbalimbali. Mafanikio haya ni ya juu zaidi! ❤️ Umeshinda vizuizi vingi na umepitia nyakati ngumu hadi kufikia hapo ulipo sasa. Umeuonyesha ulimwengu nini maana ya kujitolea kwa kweli.”

Mtaalamu huyo wa Mawasiliano ambaye ameolewa na wakili maarufu nchini Kenya, Steve Ogolla alimtambua Akothee hadharani kama dadake kipenzi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu akimpongeza kwa ufaulu huo wa masomo.

“Wacha wakati wako ujao ujazwe na fursa zisizo na mwisho, furaha, na mafanikio. Unastahili kweli. Nitakupenda na kukuthamini daima. Endelea, hujachelewa kuanza tena❤️,” aliandika.

Licha ya kuwa ndugu, Cebbie Koks na Akothee hawajawa katika uhusiano mzuri katika miaka michache iliyopita kutokana na mizozo ya kifamilia.