Baada ya kuwatania Wakenya kwa kudokeza anarejea nyumbani, Edday Nderitu afichua alikokwenda

Wengi waliamini mzazi mwenza huyo wa Samidoh alikuwa ameamua kurejea Kenya baada ya kukaa Marekani miezi kadhaa.

Muhtasari

•Edday na watoto wake walifurahia wakati katika Bustani ya Universal Studios jijini Orlando, jimbo la Florida, Marekani.

•Edday aliwachanganya wengi baada ya kuchapisha picha zake na watoto wake katika eneo lililoonekana kama uwanja wa ndege.

Edday Nderitu na Bernice Saroni
Image: INSTAGRAM// EDDAY NDERITU

Mke wa kwanza wa staa wa Mugithi Samidoh, Bi Edday Nderitu na watoto wake watatu walifurahia wakati katika Bustani ya mandhari ya Universal Studios katika jiji la Orlando, jimbo la Florida, Marekani.

Katika chapisho la Facebook la Jumapili asubuhi, mama huyo wa watoto watatu alifichua kwamba walikuwa na furaha nyingi katika bustani hiyo ya burudani na walifanya kumbukumbu nyingi nzuri.

Edday alionyesha picha nzuri zake na watoto wake wakifurahia katika sehemu mbalimbali za bustani hiyo ya mandhari.

"Ninahisi kushukuru sana kwa kumbukumbu zisizosahaulika tulizounda leo katika studio za Universal," Edday Nderitu alisema Jumapili asubuhi.

Taarifa hiyo ilikuja kama mshangao kwa mashabiki wake wengi ambao walikuwa na hakika kwamba alikuwa akirejea nchini Kenya kwa likizo ya Krismasi kutokana na chapisho lake la awali.

Siku ya Ijumaa, mke huyo wa kwanza wa mwimbaji Samidoh aliwachanganya wengi baada ya kuchapisha picha zake na watoto wake katika eneo lililoonekana kama uwanja wa ndege.

"Ni wakati," aliandika chini ya picha.

Wengi walisadiki kwamba mama huyo wa watoto watatu alikuwa ameamua kurejea Kenya baada ya kukaa Marekani kwa miezi kadhaa.

Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya katika chapisho la awali la Edday;-

Bitty Wamaitha: Karibu nyumbani kwa likizo mtoto wa kike.. Krismasi njema.

Eric Maina Kenya HSC: Karibu tena, sasa kunakaa kuwa moto.

Hon Elijah Kaseuseu: Karibuni nyumbani tulikuwa tumewamiss sana.

Hon Edwin Kiprotich: Beautiful mummie.. Karibu nyumbani babe.

Sharon Obongo:Kaa hapo mpenzi usirudi nyumbani.. alijifanya kuwa single.

Mwezi uliopita, mama huyo wa watoto watatu alimshukuru rafiki yake Bernice Saroni kwa kumsaidia kuhamia Marekani mapema mwaka huu.

Huku akimshukuru Saroni kwa ukarimu wake, Edday Nderitu alisema kwamba alichomfanyia hakiwezi kuelezewa kwa maneno tu.

Aidai kwamba ikiwa mhudumu huyo wa afya hangemsaidia, labda kufikia sasa angekuwa amekufa na binti yake angekuwa katika hali mbaya.

“Mungu akubariki Bernice, chochote ulichonifanyia mimi na watoto wangu ni kitu ambacho siwezi kukieleza. Binti yangu angekua rehab na mimi ningekuwa futi 6 chini,” Edday Nderitu alisema kupitia mtandao wa Tiktok.