"Usingle umeshindikana!" Diamond akanusha kumuacha Zuchu, awadhihaki maadui wa uhusiano wao

Bosi wa WCB ametoa taarifa nyingine akitangaza kwamba hawezi kuyavumilia tena maisha ya ukapera.

Muhtasari

•"Niwajulishe kwamba swala la usingle limeshindikana hivyo naendelea kula raha Hubani kwenye kisiwa na kitongoji kilekile cha karafuu," Diamond amesema.

•Amewadhihaki na kuwatupia vijembe waliotarajia mwisho wa uhusiano wake akisema kwamba watu huwa hawaachani tu hivyohivyo.

ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Boss wa lebo ya WCB Naseeb Abdul Naseeb almaarufu Diamond Platnumz amebadilisha kauli kuhusu tangazo lake la awali kuhusu hali yake ya mapenzi.

Mnamo Jumatano usiku, Diamond alitangaza kuwa sasa hayupo kwenye mahusiano yoyote, na kuzua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuanzia leo na kuendelea ningependa niwatangaze rasmi kuwa I AM SINGLE, sidate wala sina mahusiano na mwanamke yeyote," Diamond alisema katika taarifa yake.

Aliendelea kuwaomba mashabiki wakome kumhusisha na mwanamke yeyote akiahidi kutangaza hadharani mwenyewe pindi atakapopata tena mapenzi.

"Hivyo nisiwekewe mwanamke yeyote kama mwanamke wangu, itakapotokea kudate ama kuwa na mahusiano nitawajuza ama kutambulisha kama jinsi huwa nafanya kila wakati," alisema.

Tangazo hilo ambalo alitoa kwenye Instastori zake lilizua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakihisi amemalizana na Zuchu.

 Hata hivyo, mnamo Alhamisi mchana, staa huyo wa Bongo alitoa taarifa nyingine akitangaza kwamba hawezi kuvumilia maisha ya ukapera.

"Niwajulishe tu kwamba swala la usingle limeshindikana hivyo naendelea kula raha Hubani kwenye kisiwa na kitongoji kilekile cha karafuu," Simba alitangaza.

Aidha, aliwadhihaki na kuwatupia vijembe watu waliotarajia mwisho wa uhusiano wake akisema kwamba watu huwa hawaachani tu hivyohivyo.

“Wote mliokuwa mnashadadia poleni sana, siku nyingine acheni papara, mjifunze kusikiliza ata kidogo! Watu hawaachani kifala tu hivyo,” alisema.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na Wasafi Media, Mama Dangote alibainisha kuwa bosi huyo wa WCB hajawahi kumtambulisha Zuchu kama mpenzi wake.

Alibainisha kuwa anavyofahamu, binti huyo wa malkia wa taarab Khadija Kopa ni msanii tu chini ya lebo ya muziki ya Diamond Platnumz, Wasafi.

"(Diamond) hajawahi kuniletea Zuchu eti anataka kumuoa. Mimi kwanza najua Zuchu ni msanii wake," Mama Dangote alisema.

Aliongeza, "Kusema eti Zuchu ni mchumba wake sijui, kwa sababu mimi sijapeleka mahari kwa kina Zuchu wala barua. Zuchu namjua ni msanii wake. Kila siku tuko naye sijui. , najua ni msanii. Mimi ninachojua mchumba ni yule ambaye unapeleka barua na mahari."

Mama Dangote alidai kwamba mahusiano yanayodaiwa ya Diamond na msanii huyo wa kike wa WCB ni ya kuchezeana kwani hakuna taratibu za ndoa zilizofanyika.

“Kama mtu hajatoa barua, ni kutembea tu. Hiyo inaitwa kuchezeana. Huyo (Zuchu) sio mchumba, huyo ni mwanamke tu,” Mama Dangote alisema.

Pia alibainisha kuwa Zuchu si mwanamke wa kwanza kuhusishwa kimapenzi na mwanawe kwani amekuwa akidaiwa kutoka na wanawake wengine wengi waliowahi kuonekana naye katika siku za nyuma.

"Mimi najua mchumba Yule aliyeleta mahari," alisema.

Hata hivyo alisusia kujibu iwapo anaunga mkono uhusiano wa mastaa hao wawili wa bongofleva akibainisha kuwa wao wenyewe ndio wataamua.