“Nikupe nambake umuulize?” Khalwale amjibu aliyeuliza anaishi na mke namba ngapi Nairobi

Wakati wengine wanaoneshwa kuvutiwa na jina la mjukuu wake – Shindinshi – mmoja aliamua kumbughudhi Khalwale kimakusudi kwa kutaja kujua anaishi na mke nambari ngapi Nairobi.

Muhtasari

• “Ni jioni ya baridi sana jijini Nairobi. Mjukuu wangu, Austin Shindinshi Khalwale, amekuwa hapa kwa wikendi. Ni furaha iliyoje kuwa pamoja!” Khalwale aliandika.

Boni Khalwale.
Boni Khalwale.
Image: x

Katika mitandao ya kijamii, aghalabu wafuasi wa mtu maarufu huuliza maswali ya kulenga kumuaibisha kwa lengo la kujitafutia umaarufu.

Wachache sana hujibu maswali kama haya lakini katika siku za hivi karibuni, watu maarufu wamekumbatia mfumo wa kutoa majibu ya shombo vile vile ili kuwazima wachokozi wa mitandaoni.

Ndio kama hivi ambapo kiranja wa wengi katika bunge la seneti ambaye pia ni seneta wa Kakamega, Boni Khalwale alimjibu mtumizi mmoja wa mtandao wa X aliyetaka kujua maelezo ya ndani kuhusu familia yake.

Khalwale alipakia picha mbili akiwa anafurahia muda wake na mjukuu wake katika mtandao wa X akisema kwamba Nairobi kuna baridi kali na mjukuu wake alimtembelea kumalizia wikendi yake pamoja.

“Ni jioni ya baridi sana jijini Nairobi. Mjukuu wangu, Austin Shindinshi Khalwale, amekuwa hapa kwa wikendi. Ni furaha iliyoje kuwa pamoja!” Khalwale aliandika.

Wakati wengine wanaoneshwa kuvutiwa na jina la mjukuu wake – Shindinshi – mmoja aliamua kumbughudhi Khalwale kimakusudi kwa kutaja kujua anaishi na mke nambari ngapi Nairobi.

Khalwale naye hakutaka kusalia na wafungwa, aliamua kuachia mshale wa sumu kwa mtumizi huyo kwa kumjibu kwamba mwenyewe asingeweza kumjibu, labda tu ampe namba ya mkewe huyo anayeishi naye Nairobi ili ajue mwenyewe kutoka kwa mhusika kuwa ni nambari ngapi kwa Khalwale.

“Nairobi unakaa na bibi namba ngapi kiongos?” @jedyke alimuuliza.

“Ninaweza nikakupa namba yake umuulize?” Khalwale alimjibu na kuzua vichekesho kutoka kwa baadhi ya watu.

Wengine walimshabikia Khalwale kwa jibu hilo huku wengine wakimtania kwamba hafai kuwa mkali hivyo kwa wafuasi wake.