logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto mrembo akitembea na bango barabarani kuombe pesa za kununua sodo (video)

Baadhi walitaka suala la taulo za usafi wakati wa hedhi kuwa la bila malipo kwa kina dada.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku30 January 2024 - 09:00

Muhtasari


• Kuelekea mwisho wa video, bibi huyo alionekana ndani ya duka, akinunua pakiti mbili za pedi kwa pesa alizopokea.

Msichana akiomba msaada wa sodo.

Msichana mmoja amezua hisia mseto katika mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye video akitembea itaani huku ameinua bango lenye ujumbe wa kuomba wahisani kumsaidia na hela za kununua sodo.

Mrembo huyo mwenye umri wa makamo alikuwa akizunguka na bango hilo lenye ujumbe huo wa kuvutia hisia za huruma kwa ajili ya kuomba msaada wa kujisitiri nyakati za hedhi.

Katika video iliyoenea mtandaoni, mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la @meyiwa_vera, alivamia mtaa huo usiojulikana akiwa na bango kubwa, akitangaza hitaji lake la haraka la fedha za kununulia taulo hizo za kujisitiri.

Bango hilo linasomeka, ‘Need money for pads’, na kuwarahisishia wapita njia kutambua hitaji lake la bidhaa za usafi wa hedhi.

Bibi huyo anaonekana kutoogopa alipokuwa akiwaendea watu barabarani, akiwaomba pesa. Wengi walimpa pesa.

Kuelekea mwisho wa video, bibi huyo alionekana ndani ya duka, akinunua pakiti mbili za pedi kwa pesa alizopokea.

Yeye, basi, alipakia kila bidhaa ndani ya nailoni, akizisambaza kati ya wanawake aliowakuta barabarani.

Tazama video hapa chini:

Video hiyo imevutia hisia za huruma kutoka kwa baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii, baadhi wakihisi kwamba suala la taulo za usafi wakati wa hedhi linafaa kupewa kipaumbele na serikali yoyote ili kwamba ziwe zinatolewa bila malipo kwa wasichana waliobalehe.

“Taulo za usafi wa hedhi zinapaswa kufanywa bure na kondomu zinapaswa kuwa ghali” prankihottie.

“Kwa nini naona hii inasumbua” vivianofgrace.

“Ingekuwa bora kama angeenda shule ya umma kushiriki pedi. Alifanya vizuri!” tohirat_couture.

“Unaona wanawake walitoa zaidi? Tunaelewa uchungu” perfect_aster.

Nchini Kenya, seneta maalum Gloria Orwoba mwaka jana alianzisha vuguvugu la kuchangisha sodo kwa ajili ya kuzigawa kwa wasichana waliobalehe ambao hawana namna ya kupata bidhaa hizo za usafi wakati wa hedhi.

Mnamo mwezi Mei, mwanasiasa huyo kijana alizindua "Glo's Pad Bank" kontena la futi 20 lililolengwa kukusanya pedi za usafi na kusambazwa kote nchini kando na kuzindua muswada wake unaoitwa Utoaji wa Taulo za Bure za Usafi kwa ushiriki wa umma.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved