Askofu mkuu adai mbele ya waumini kuwa alienda mbinguni na kukaa saa 1 dakika 45 (video)

Hii si mara ya kwanza kwa mtumishi wa Mungu kusikika akihubiri baadhi ya mambo ambayo wengi haswa katika muktadha wa mitaani wanasema ni ‘stori za jaba’.

Muhtasari

• Kulingana na yeye, roho yake ilitolewa nje ya mwili wake kwa uzoefu huo mara moja katika maisha.

• Ilikuwa ni rekodi ya ibada yake ya Jumapili alipofanya ufunuo.

Mwanzilishi wa kanisa la Action Chapel Ministries.
Archbishop Nicholas Duncan-Williams// Mwanzilishi wa kanisa la Action Chapel Ministries.
Image: Facebook

Askofu Mkuu anayefahamika kwa jina Duncan Williams kutoka nchini Ghana amewazuzua waumini katika kanisa lake baada ya kutoa ushuhuda kanisani kwamba alikwenda mbinguni na kutumia muda wa saa 1 na dakika 45 akiwa na Mungu.

Kauli hii kutoka kwa mtu wa Mungu anayeheshimika tangu wakati huo imezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii huko Afrika Magharibi huku watumiaji wa mtandao wakiwa hawajali kuhusu hilo.

Katika video hiyo, Duncan Williams anaweza kuonekana na kusikika akisimulia wakati alipokuwepo Mbinguni kwa saa moja na dakika 45.

Kulingana na yeye, roho yake ilitolewa nje ya mwili wake kwa uzoefu huo mara moja katika maisha.

Ilikuwa ni rekodi ya ibada yake ya Jumapili alipofanya ufunuo.

 

Mwanzilishi na mwangalizi mkuu wa Action Chapel International alisema;

“Nilipoenda Mbinguni… nilikwenda Mbinguni kwa muda wa saa 1 na dakika 45, nilitolewa nje ya mwili wangu hadi Mbinguni kwa muda wa saa 1 na dakika 45 na nikaona mambo ya kuvutia sana…Malaika akaniletea mlima mrefu na nyasi ilikuwa kama almasi…”

Tazama video hapa chini kujua zaidi...

Hii si mara ya kwanza kwa mtumishi wa Mungu kusikika akihubiri baadhi ya mambo ambayo wengi haswa katika muktadha wa mitaani wanasema ni ‘stori za jaba’.

 Miezi miwili iliyopita, Radiojambo.co.ke iliripoti kuhusu mchungaji mmoja kutoka nchini Uganda ambaye alidai kwamba aliwahi kumezwa na kutemwa na simba baada ya kama dakika 45 hivi.

Nabii William Ssozi anaonekana akifafanua kuwa alimezwa na Simba akiwa katika siku zake za mwanzo za Utumishi katika sehemu moja ya Afrika Kusini na anaendelea kusema kuwa ni kwenye tumbo la simba ambapo alijifunza kutabiri.

“Nchini Afrika Kusini ndiko nilishuhudia kitu cha kunibadilisha kabisa kimaisha. Nilimezwa na simba. Tulikuwa tumeenda kutembea mbugani, na gari letu liliisha mafuta katikati ya mbuga. Sijui vile ilitokea lakini tulianza kusikia sauti za simba na tuliogopa sana. Waliniambia mimi ndio mchungaji niwaweke kwa maombi.”

“Simba akaja na kati ya marafiki zangu wote, simba alinichagua mimi tu na kunimeza. Na tumboni mwa simba ndipo Mungu alinijia na kunizungumzia, na kuniambia jinsi nitakavyoanza kutoa unabii kwa undani Zaidi,” aliongeza.

"Nilikuwa na shule yangu ya Unabii katika tumbo la simba."